27 views 2 mins 0 comments

CHUO CHA KODI IMEOMBWA KUFANYA MAFUNZO YA KODI NA FORODHA ILI  KUONGEZA MAKUSANYO YA KODI KITAIFA

In BIASHARA
November 22, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Serikali kupitia Wizara ya Fedha imesema  inatambua mchango wa chuo cha kodi kwenye kutoa mafunzo ya kodi na forodha hivyo kuongeza makusanyo ya kodi kwenye Taifa.

Hayo ameyasema  leo  jijini dar es salaam Naibu  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akimwakilisha Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kwenye Mahafali ya kumi na saba kwenye chuo cha kodi (ITA)  ambapo wamehitimu jumla ya wahitimu 417.

Elijah amesema Chuo kijikite na tafiti zitakazotoa changamoto kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi huku mapendekezo mengi kwenye tafiti yanakosa utafiti kwenye jamii hivyo yataleta mapendekezo na tafiti kwenye kufikia malengo wanayoyataka.

Aidha Elijah Amewasisitiza Chuo kiendelee kutoa mafunzo ya viwango vya juu kuzingatia kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani ndipo dunia inapoelekea kwa sasa.



Amesema Chuo kijikite na tafiti zitakazotoa changamoto kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi huku mapendekezo mengi kwenye tafiti yanakosa utafiti kwenye jamii hivyo yataleta mapendekezo na tafiti kwenye kufikia malengo wanayoyataka.

Awali akiongea Prof.Isaya Jairo Mkuu wa Chuo cha Kodi Mamlaka ya mapato Tanzania (ITA) amesema Chuo kimetengeneza wataalamu wengi wa forodha ya kodi  yenye misingi ya kujenga umahiri kwenye kukuza uchumi wa Taifa pamoja na kutumia fursa za uendeshaji wa teknolojia na sayansi wa sasa ambapo itawasaidia wahitimu hao waendane na kasi ya teknolojia na forodha ya dunia ya sasa.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Kodi Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema baraza lililopo liendelee kufanya kazi  ili kufanikisha watumishi ambapo itawezesha kuongeza idadi ya walipa kodi pamoja na kuongeza ulipaji kodi kwa nchi na  wataendelea kuboresha miundombinu ili watoe wahitimu bora kwa maendeleo ya nchi.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram