19 views 2 mins 0 comments

NAIBU WAZIRI SANGU AMPIGIA CHAPUO RAIS SAMIA,AWATAKA WANANCHI KUICHAGUA CCM JIMBONI KWELA

In KITAIFA
November 22, 2024



Na Mwandishi Wetu – Rukwa.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na  Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwela ametoa wito kwa Wananchi  kuendelea  kumuunga mkono Rais, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan  kwa kuwachagua  Viongozi wa Serikali za Mitaa wa Chama Cha Mapinduzi.

Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati akifanya Mikutano ya Kimkakati ya kumuunga mkono  Rais Mhe.Samia Suluhu Hasan ya kuwachagua  Viongozi katika Kata ya Mfinga, Kalumbaleza, Mwadui na Muze zilizopo katika Jimbo la Kwela, Mkoani Rukwa.

Amesema CCM ina kila sababu ya kushinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa jinsi ilivyojimbanua kushughulikia kero zinazowakabili wananchi wa Jimbo hilo.

Amesema wananchi wa Jimbo hilo wana kila sababu ya kuwapigia kura viongozi wa Serikali za Mitaa waliogombea kupitia chama hicho ikiwa ni ishara ya shukrani kutokana na mabilioni ya fedha ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anayoyatoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika  Jimbo hilo.

” Tumejiandaa vilivyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa  kwa kuhakikisha  tunashinda  kwa kishindo ” amesisitiza Mhe.Sangu

Amesema katika kipindi chake cha Uongozi Mkoa wa Rukwa hususan Jimbo la Kwela  limefunguka ambapo kila kona barabara zimeboreshwa huku zingine zikiendelea kuwekwa lami ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.

Amesema huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, umeme pamoja maji zimeimarika ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Diwani wa Muze, Mhe.Kalolo Ntalli amesema kwa jinsi walivyojipanga na kutokana na ubora wa wagombea waliopitishwa na Chama  hicho, hakika ushindi ifikapo tarehe 27 Novemba mwaka huu hauepukiki.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram