22 views 10 secs 0 comments

KIKOSI KAZI MAALUM KUUNDWA, KUFUATILIA WAHALIFU MAKOSA YA MTANDAONI.

In KITAIFA
November 23, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Na Mwandishi wetu – Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa,  wakutana na wadau wa mawasiliano yakiwemo makampuni ya simu kujadili kuhusu Makosa ya uhalifu wa mtandaoni mkutano huo umefanyika leo Novemba 22, 2024 Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dar es Salaam.



Pamoja na mambo mengine Kikao kicho kimeazimia kuunda Kikosi Kazi Maalum kitakacho shirikisha wajumbe mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na kutoka Wizara hizo mbili ili kufuatilia  makosa yote ya uhalifu wa mtandaoni.



Mkutano huo pia umehudhuriwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania  (BoT) Bi. Sauda  Msemo, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari,  DCI. Ramadhan Kingai, DPP. Sylvester Mwakitalu na wataalamu wengine kutoka TCRA.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram