16 views 13 secs 0 comments

NAIBU WAZIRI SANGU APIGA KURA KIJIJINI KWAKE , AWAHIMIZA WANANCHI

In KITAIFA
November 27, 2024



Na Mwandishi Wetu-Rukwa

Naibu Waziri, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ma Utawala Bora Mhe.Deus Sangu  amesisitiza umuhimu wa Wananchi wa Jimbo la Kwela kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku akibainisha kuwa uchaguzi huu ni fursa kwa wananchi kupata viongozi wa karibu wanaojua  changamoto zinazowakabili  za moja kwa moja katika maeneo yao.

Mhe.Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela ametoa kauli hiyo  mapema leo Jumatano Novemba 27, 2024 mara  baada ya kumaliza kupiga kura katika Kitongoji cha Pokopoko Kata ya Laela Mkoani Rukwa

Akiwa ameonesha kuridhika na idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika kitongoji hicho na jinsi mchakato wa uchaguzi unavyoendelea, Mhe.Sangu  amewataka Wananchi waliobaki kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura.


Amesisitiza kuwa ushiriki wa kila raia ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanikiwa kwa haki na uwazi, huku akiwapongeza wale ambao tayari wamepiga kura kwa kuwa mfano mzuri wa uzalendo.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram