11 views 2 mins 0 comments

FCC IMEDHAMIRIA KUTOA ELIMU KWA WATANZANIA NAMNA YA KUFANYA BIASHARA BILA KUDIDIMIZA SERA

In BIASHARA
November 30, 2024

Na Madina Mohammed WAMACHINGA

Tume ya Ushindani (FCC) imedhamiria kutoa elimu kwa Watanzania juu ya namna nzuri ya kufanya biashara bila kudidimiza sera na taratibu za ushindani za ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Novemba 29, 2024 Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio na waandishi wa habari katika ofisi za taasisi hiyo mkoani Salaam, ambapo FCC imezindua Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Ushindani Duniani ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 8 Desemba, 2024.


Amesema ili kufanyika kwa biashara katika mazingira ya haki na usawa, ni muhimu kuwa na udhibiti kupitia sera na sheria akitolea mfano mikataba yote inayokinza na ushindani, na miungano yote ya kampuni ambayo inafifisha ushindani.

Hata hivyo Erio amesema kuwa licha ya nchi kuwa na misingi ya biashara huria, kuna utofauti wa rasilimali kutoka kwa wafanyabiashara ambapo wakifanya biashara katika misingi hiyo bila utaratibu wa aina yoyote, watu au kampuni zitaumia kwa kushindwa kupata fursa sawa ya kufanya biashara.

โ€œKuna mbinu nyingi chafu zinaweza kutumika kwenye utendaji wa biashara, mfano wafanyabiashara kuwaondoa washindani wao sokoni ili wabaki peke yao, kwa sababu kwani mfanyabiashara yeyote lengo lake ni kupata faida, sasa mkiwa wengi faida itapungua ingawa ufanisi na upatikanaji wa bidhaa utaongezeka,hiviyo anaweza kuamua kwa makusudi kabisa kufanya vitu ambavyo vinafifisha ushindani na kwa nguvu yake ya kifedha, rasilimali watu au utaalamu akawasababisha wengine kushindwa kufanya biashara sokoni na kuondokaโ€, amesema Mkurugenzi.


Amesema changamoto zote hizo zinatokanazo ni kutokuwa na usawa kwa wafanyabiashara hao hivyo amesema kama taasisi ya FCC ni kutengeneza mazingira sawia ya watu wote kufanya biashara kwa usawa kupitia sera na sheria.

Aidha Kilele cha maadhimisho hayo itakuwa 5 De semba 2024 katika Hoteli ya Golden Tulip, Oysterbay, Dar es Salaam ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Kilele hicho kitaambatana na kongamano litakalowakutanisha magwiji wa sheria na biashara ambao watajadili mazingira ya biashara na ushindani Tanzania na watapata fursa ya kuishauri FCC juu ya namna nzuri ya kutekeleza majukumu yake.

Maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Ushindani Duniani, kaulimbiu โ€˜Sera ya Ushindani na Kudhibiti Kukosekana kwa Usawa katika Uchumiโ€™.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram