74 views 2 mins 0 comments

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KUAMULIWA LEO

In KITAIFA
December 03, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-DAR ES SALAAM

NI kampeni za lala salama. Ndivyo unaweza kusema, hasa baada ya vyama vya siasa nchini kupepetana kwa siku saba kwenye majukwaa ya kisiasa kusaka ushawishi kwa wananchi.

Kutokana na hali hiyo sasa Watanzania leo wataamua kwa kupiga kura ili kuchagua wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji huku CCM ikitamba kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo.

Kutokana na hali hiyo timu wa wabunge na madiwani wote wa CCM sasa imepiga kambi kwenye majimbo ili kusaka kura ambapo Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) akiwa katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa jimbo la Ubungo, alisema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ndiyo sababu ya wananchi kuchagua Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni, Prof. Kitila alisema miongoni mwa mambo muhimu katika kuchagua ni kuangalia chama ambacho ni imara jambo ambalo CCM inazo sifa hizo.

“Tunachagua mambo manne na tupo katika mfumo wa vyama vingi wa ushindani, kwa hiyo tunapochagua na wenzetu na tunapima kwa kuzingatia mambo manne. Jambo la kwanza, tunaangalia chama, chama ndio huzaa Serikali, ukiwa na chama cha ovyo kinazaa Serikali ya ovyo, chama imara huzaa Serikali imara,” alisema Prof. Kitila.

Aidha, alisema katika kila eneo yapo mambo yaliyoahidiwa na kutekelezwa huku akitolea mfano ujenzi wa machinjio katika soko la Manzese na ujenzi wa jengo la flemu za maduka katika soko la Manzese ambalo lipo mbioni kukamilika na ujenzi wa Zahanati ambao utaanza hivi karibuni na tayari eneo limepatikana na fidia imelipwa.

/ Published posts: 1715

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram