38 views 3 mins 0 comments

TCCIA NA CHEMBA YA KIMATAIFA YA DUBAI KUSHIRIKIANA KATIKA BIASHARA NA UWEKEZAJI

In KITAIFA
December 12, 2024

Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Suleiman Jafo amewaomba wawekezaji kutoka nchi za falme za kiarabu kuja kuwekeza Nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo Biashara.

Jafo ametoa rai hiyo leo Desemba 12,2024 wakati wa utiliaji saini hati ya Makubaliano ya Biashara na  Uwekezaji kati ya Tanzania na Nchi za kiarabu kupitia Chemba ya Biashara ,Viwanda na kilimo ( TCCIA) pamoja na Chemba ya Kimataifa ya Dubai.



Aidha amesema kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi za kutosha kufanya uwekezaji ikiwemo sekta ya Kilimo,Madini,Utalii na hata Miundombinu, hivyo amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na nchi za falume za kiarabu itasaidia kuinua uchumi pamoja na kuleta ajira kwa Vijana wa kitanzania kutokana na uwekezaji utakaofanywa na Nchi hizo.

“Tanzania tuna Mazingira mazuri  ya uwekezaji kutokana na rasilimali nyingi tulizo nazo pamoja na maeneo ya Utalii,mfano 2027 kuna mashindano ya AFCON tumewaalika waje wawekeze kwenye mahoteli na majumba mazuri ya kulala wageni,hivyo ni fursa nzuri kwa nchi yetu” amesema Jafo



Nakuongeza” kwahiyo binafsi sisi kama Tanzania tumejipanga kuhakikisha tunawavutia watu wengi sana kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza Nchini Tanazia na hii ni dhamira ya dhati ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuvutia uwekezaji.

Aidha amesema kuwa kwa sasa ushirikiano wa  Biashara kati ya Tanzania na Dubai unaendelea vizuri ambapo kwa takwimu za mwaka 2022 Tanzania imeuza bidhaa za kiasi cha Dola bilioni 1.2 nchini Dubai.



Kwa upande wake rais wa TCCIA Vincent Minja amesema kwamba wameingia makubaliano kati ya Chemba yake  na Chemba ya Dubai kutokana na kwamba Dubai ni kubwa sana hapa mashariki ya kati katika masuala ya Biashara.

“Kusaini kwa makubaliano haya leo itawasaidia sana wafanyabiashara wa Tanzania  kuweza kuingia kwenye masoko ya dunia kupitia nchi ya Dubai kwasababu Dubai sio kwamba ni lango tu la kupitishia biashara bali  ni kituo cha Soko la biashara  kwakuwa dunia nzima wananunua bidhaa zao kupitia nchi hiyo.



Aidha Minja amezitaja sekta ambazo zimepewa  kipaumbele kwenye uwekezaji huo kua  ni Kilimo,Madini, Nishati pamoja na Utalii kwasababu kwa sababu sekta hizo zinapatikana hapa Nchini.

“Tupo karibu na wenzetu wa Dubai hapa Nchini,tuna wawakilishi wao ndio maana tupo nao hapa kwa ajili ya kushirikiana pamoja katika masuala ya biashara na uwekezaji.” Amesisitiza Minja kwenye Mkutano na Wanahabari.

/ Published posts: 1636

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram