46 views 2 mins 0 comments

RC CHALAMILA TUSIWE WEPESI KUHUKUMU MAKOSA YA MTU BILA KUJUA HISTORIA YAKE

In KITAIFA
December 13, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-Asema Manabii na Viongozi wengine wa Dini wana nafasi kubwa katika Jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Disemba 12 amehudhuria mkutano wa kila mwaka wa Kitaifa wa viongozi wa kiroho ( The Annual National Leaders Prophetic Meeting) uliofanyika katika ukumbi wa The Supper Dom Masaki akiwa mgeni rasmi.

Akiongea na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano huo RC Chalmila alisema katika maisha ya kila siku tusiwe wepesi wa kuhukumu makosa ya mtu yeyote pasipo kujua historia yake kwa kuwa kila mmoja wetu amezaliwa na kupata makuzi katika mazingira tofauti, yuko ambaye kazaliwa na kupata makuzi katika mazingira ya kidini na mwingine mazingira ya wizi ” Kule njombe mtu anazaliwa haijui kabisa chai, lakini anaujua ulanzi na anakunywa” Aliseama RC Chalamila

Hivyo viongozi wa Dini ndio watu walioko katika mazingira salama zaidi na wana msaada mkubwa katika kuibadilisha jamii dhidi ya mienendo na tabiaย  zisizofaa ambapo ametoa wito kwa kila mmoja katika maisha ya kila siku ni vizuri kuchimba historia ya mtu kabla ya kumhukumu.

Aidha Mkutano huo wa kiroho licha ya kuwa na viongozi mbalimbali wa Dini hapa nchini umehudhuliwa na Prophet Elvis Mbonye kutoka Nchi ya Uganda ambaye alipata wasaa wakuliombea Taifa la Tanzania pamoja na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani.

Mwisho RC Chalamila ametoa rai kwa viongozi wa Dini kupitia kongamano hilo kumwombea Mhe Rais Dkt Samia ili aendelee kuliongoza vyemaย  Taifa la Tanzania kwa masilahi mapana umma na ustawi wa jamii kwa ujumla.

/ Published posts: 1636

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram