Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameainisha matukio kadhaa yaliyogusa mkoa huu mwaka 2024, akisisitiza juhudi za mamlaka kurejesha utulivu na kuboresha usalama.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Disemba 23,2024 Chalamila amesema matukio hayo yameathiri mkoa kwa namna tofauti, lakini juhudi za pamoja za serikali na wananchi zimechangia kutatua changamoto hizo kwa mafanikio.
Amefafanua kuhusiana na matukio matatu makubwa yaliyozia taharuki,likiwemo la Bwana harusi Vincent Peter Masawe mkazi Wa kigamboni aliyedaiwa kurejea na baadae kugundulikabkuwa alijificha mwenyewe kutokana na madeni yaliyokuwa yakimkabili kutoka Katika Mabenki na watu mbalimbali ambaye jeshi la polisi lilifanikiwa kumpata alikukuwa amejificha.
Chalamila ameeleza tukio lililoibua hofu kubwa, ambapo mtoto mdogo alipotea na kuhisiwa kutekwa ambapo uchunguzi wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwa mtoto huyo alikuwa ametumbukia ndani ya kisima Cha maji, alisema Chalamila.
Pia amefafanua kuhusu tukio la mfanya biashara aliyejulikana kwa jina la Daisle Ulomi mfanya biashara Wa sinza ambaye alidaiwa kutekwa na kuuawa Chalamila amesema kuwa Ulomi hakutekwa Bali alipata ajali ya pikipiki na kusaidiwa na wasamalia kupelekea Hospitali ambapo alifariki na kutokana na kuwa hakuwa na kitambulisho chochote ilikuwa vigimubkuwapata ndugu zake hivyo mwili ukawekwa Katika chumba Cha kuhifadhia maiti Katika Hospitali ya mwananyamala
“Kuna watu wakauliza kwanini apelekwe Hospitali bila polisi kupewa taarifa? Jeshi la Polisi limeelekeza kuwa majeruhi wanapaswa kupatiwa matibabu haraka bila kuhitaji fomu ya PF3, ili kuokoa maisha, Ni muhimu wananchi kuelewa kuwa utaratibu huu unalenga kuokoa maisha ya majeruhi, na sio kuwachelewesha kwa sababu ya taratibu za nyaraka,” alisema.
Akizungumzia sakata la kutekwa Kwa Abdul Nondo na kifo Cha Ally Kibao Chalamila amebainisha kuwa taarifa za kutekwa kwake zilileta mkanganyiko, baada ya watu waliodhaniwa kuwa polisi kutumia pingu wakati wa tukio. Amesema maafisa wa polisi wameagizwa kuhakikisha wanavaa sare rasmi wanapotekeleza majukumu yao ili kuepusha mkanganyiko na lawama zisizo za msingi.
Ametoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha wanatembea na vitambulisho vya taifa (NIDA) ili kurahisisha utambuzi na kusaidia mamlaka wanapokutana na changamoto.
“Kutokuwa na kitambulisho mara nyingi kunaleta changamoto katika kuwasaidia wananchi wanapopatwa na matatizo. Ni vyema kila mmoja ajitahidi kuwa nacho,” alisisitiza