35 views 5 mins 0 comments

NI WASIRA CCM

In KITAIFA
January 20, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-DODOMA

NI Stephen Wasira CCM! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mqpinduzi(CCM) kupitisha jina lake kuwa Makamu Mwenyekiti akichukua nafasi iliyoachwa na Abdulrahman Kinana.

Wasira amepitishwa katika mkutano huo uliofanyika jana  mjihi Dodoma ambapo amepata kura za ndiyo 1,910 kati ya kura halali 1,917 huku saba zikisema hapana na hivyo amepata ushindi wa asilimia 99.42.

Akizungumza baada ya kupitishwa katikak mkutano guo uliofanyika chini ya Mwenyekiti  wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , Wasira alisema anawashukuru wajumbe wa mkutano huo kupitisha jina  lake na kwamba anaamini Mungu amemtumia Rais Samia kuwa katika nafasi hiyo ambayo hakuwa anafikiria kuwa ataitumikia.

Wasira alisema kuwa  kazi ya kwanza atakayoanza nayo ni kuhakikisha CCM kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwani malengo makuu ya Chama hicho ni kuendelea kushika dola.

“CCM ina kila sababu ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo kwani Mwenyekiti wa Chama Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametekeleza vyema Ilani uchaguzi Mkuu katika sekta mbalimbali na kusisitiza kazi ya CCM imeelezwa katika Ibara ya 5 ya Katiba ya chama hicho chenye ushawishi mkubwa kisiasa barani Afrika.

Aliongeza kuwa katika  Ibara ya 5 ya Katiba ya CCM inaeleza kuwa Chama kinawajibu wa kushinda uchaguzi na kukamata dola kazi ambayo katika uchaguzi.”Kazi tuliyonayo ni kukamata dola ya muungano na Zanzibar.”

Alitumia nafasi hiyo kufafanua kwa kazi ambayo imefanyika katika kutekeleza Ilani pamoja na ahadi zake kwa Watanzania uhakika wa kushika dola ni mkubwa na hawana shaka katika hilo.

“Tunashuhudia kukamilika kwa miradi mbalimbali ikiwemo ya kujengwa miundombibu ya afya,maji ,elimu,barabara na katika reli ya mwendo kasi hivi sasa safari za kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma zinaendelea na ujenzi wa reli hiyo kuelekea Kigoma unaendelea.” Alisema.

Pamoja na hayo Wasira alisema Rais Samia kupitia falsafa 4R aliyoiasisi ambayo moja ya ajenda zake ni maridhiano, hivyo kupitia nafasi ya Makamu Mwenyekiti atahakikisha ataendeleza ajenda hiyo.

Alitumia nafasi hiyo kusisitiza kuwa Chama Cha Maoinduzi kitaendelea kusimamia amani,umoja na mshikamano ,hivyo alisema kama kuna Chama kipo hapa nchini na kinataka vita CCM haitakwenda huko itaendelea kusimamia amani.

Awali akitangaza matokeo ya kura hizo, Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson alisema Wasira ameibuka na ushindi kwa kupata asilimia 99.42.”Idadi ya kura zilikuwa 1,921, zilizoharibika ni kura nne, kura halali 1,917, kura za hapana saba huku kura za ndiyo ni 1,910 sawa na asilimia 99.42.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Rais Dk. Samia alimtangaza Wassira kuwa amechaguliwa kurithi nafasi ya Kinana na wakati akitangazwa ukumbi mzima ulipuka kwa shangwe.

VIONGOZI WAMUELEZEA

Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda alisema  Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wassira ni kiongozi mwenye uzoefu wa kutosha katika njanja za kisiasa hivyo atakisaidia  Chama hicho kuendelea kushika dola.

Pinda alisema kuwa anamjua Wassira kama kada mahiri katika Chama hicho na aliposoma historia yake ilimshutua kumbe sio kama alivyokuwa anamfikiria kwani aliibuka tangu enzi za TANU mwaka 1959.

Alisema kuwa Wasira alipata kadi ya uanachama akiwa na miaka 16 na amekuwa kwenye nafasi mbalimbali na kote huko ameonesha uwezo mkubwa kichama na shughuli za serikali kwa ujumla.

Wakati huo huo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana alimpongeza Wassira kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na kwamba amewahi kufanya kazi na Wasira na hakika ni mtu hodari, mwadilifu.

Akisoma Azimio la Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuhusu wasifu wa Wassira, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mohammed Said Dimwa, alisema katika kikao cha NEC kilichofanyika juzi kilimteua Wassira baada ya kujiridhisha juu ya tabia, mwenendo na sifa zake katika Chama.

Alisema Wassira ni muumini wa kweli wa siasa za chama chao cha ujamaa na kujitegemea, anazingatia kikamilifu masharti ya wanachama, sifa na miiko ya kiongozi kama ilivyoainishwa katika Katiba ya CCM na daima amekuwa mstari wa mbele kupigania na kulinda maslahi ya chama hicho.

“Wassira ni mkweli, mnyenyekevu, anapenda nchi yake, raia mwema wa Tanzania, muumini wa muungano katika serikali mbili, mwanamapinduzi anayependa maendeleo ya nchi na kuchukia rushwa kwa vitendo.”

/ Published posts: 1715

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram