48 views 2 mins 0 comments

AZAM MEDIA NA TRACE GROUP WAINGIA MAKUBALIANO KWA URUSHAJI MATANGAZO ZA TUZO ZA TRACE FEBRUARI 26

In BURUDANI
January 21, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Kampuni ya Azam Media Limited imesaini mkataba wa makubaliano na Trace Group inayondaa tuzo za Trace kwa ajili ya urushaji matangazo ya usiku wa tuzo hizo Februari 26, 2025.



Mkataba huo umesainiwa na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Azam Media Limited, divisheni ya Maudhui na Utangazaji @yahyamohamedtz pamoja na Mkuu wa maudhui Trace Awards, Valerie Gilles- Alexia.

Mohammed Amesema Tuzo za TRACE kwetu sisi (Azam Media ) ni kipimo na ni mita ya sisi kujipima na kuzifanya Kwa ubora.



“Tunauwezo mkubwa wa Kuendelea kutimiza wajibu Wetu huo wa Kuendelea kuwahakikishia sanaa ya kitanzania kupata nafasi kuwa kimataifa na kuvutia vijana wengi wa kitanzania kuingia Katika Sanaa hiyo ya kimziki na kuufanya mziki kama sehemu ya ajira rasmi ya biashara ambayo inaweza Kuendelea kufanya taifa letu Kuendelea kufurahia mapato haya pia Kuendelea kuvutia mataasisi yenginezo pia kuona nafasi kubwa ya kufanya Tanzania kuwa ni myumbani kwao”. Amesema Mohammed



Ameongeza kuwa Kwa kufanya matukio makubwa kama haya na Trace imetupa heshima Kwa watanzania Kwa kuleta tukio kubwa hili la Awards 2025 Katika visiwa vya ZANZIBAR

Nae Mkuu wa maudhui Trace Awards, Valerie Gilles- Alexia akieleza sababu. Za kuingia makubariano na Azam media Amesema kuwa lilikuwa ni jambo la wazi kabisa kwamba tungefanya kazi na Azam media, Amesema kuwa”sisi ni washirika na Azam”.



Valeri amezungumzia pia ubora na umahiri wa Azam Media sio tu ndani ya nchi, hata Afrika kwa ujumla, pia amezungumzia ushirikiano wa kampuni hizo mbili wa zaidi ya miaka 8 sasa.

Pia Mwakilishi wa Trace Awards Tanzania, @sevenmosha akieleza kwa undani kuwa hizi ndizo Tuzo zinazojulikana kutoka afrika,nafasi Kwa ‘bongo fleva’ kujulikana,lazima tuioneshe dunia tunaweza

/ Published posts: 1715

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram