
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
-DODOMA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kipi kwenye hesabu kali hasa baada ya kukamilisha uteuzi wa wagombea wake wa urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (CCM)
Hatua hiyo ya kufanya uteuzi wa wagombea wake mapema unakwenda kuakisi kwamba chama hicho tawala nchini, kimedhamiria kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni pamoja na kupata muda wa kupanga mikakati ya ndani ya chama na nje katika kukabiliana na wagombea wa vyama vya upinzani watakaoteuliwa kuwania urais.
Kutokana na hali hiyo juzi CCM ilimteua Rais Dkt. Saia Suluhu Hassa kuwa mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu huku naye Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi akiteuliwa kuwa mgombea wa Urais wa Zanibar waka mwaka 2025-2030.
Hatua hiyo ya kufikia uamuzi wa kutaka kuwapitisha kuwa wagombea wa urais kwa upande wa Bara na Zanzibar kama njia muhimu ya kukifanya chama kijipange na ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Katika hoja hiyo iliyowasilishwa na na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa ambapo aliungwa mkono na wajumbe wengine na kulazimika kuandaliwa azimio ambalo liliitaka Halmaahauri Kuu ya Taifa ya CCM kwenda kukutana na kuandaa azimio ambalo lilikubaliwa na kisha kufuta utaratibu ikiwamo kuandaliwa kwa vikao na kisha mkutano Mkuu kulazimika kupiga kura.
Kutokana na hali hiyo ilimlazimu Rais Dkt. Samia kutoka ukumbini na kumuachiwa kiti Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye baada ya kukamilisha mchakato huo wa upigaji kura uliosimamiwa na Mwenyekiti wake Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
Hata hivyo baada ya kukamilika kwa mchakato huo, Dkt Mwinyi alitangaza matokeo na kumtangaza Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata kura 1924 ambazo ni sawa na asiliamia 100 ambapo hakukuwa na kura ya Hapana wala iliyoharibika.
Baada ya kukamilisha hatua hiyo, akiendesha kikao hicho Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, aliwashukuru wajumbe kwa kuendelea kumuamini huku akiwaomba wawe na utulivu na kuwataka wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kwenda kwenye kikao na kujadili suala la nani mgombea mwenza.
Kikao hicho cha Kamati Kuu, kilikwenda kufanyika kwa muda wa dakika 40 na baada ya hapo walirejea ukumbini ndipo alipoingia Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Samia.
“Tumekamilisha mchakato awali huku nyuma alikuja kuniambia Dkt. Philip Mpango kuwa anahitaji kupumzika ili aweze kuishi zaidi, kwani sasa ana miaka 68 na mama yake ana aliishi miaka 86 na yeye anataka kuishi zaidi ya hapo. Alipoona hivyo sijamjibu wiki iliyopita aliniandikia barua nayo sijamjibu na hili nimewashirikisha kaka zangu hawa watatu ( Jakaya Kikwete, Dkt Ali Mohamed Shein na Dkt Aman Karume.
“Baada ya majadiliano ya kina ya nani anaweza kuwa mgombea mwenza, nao waliweza kujadili na leo (jana) tumejadili kwenye kamati kuu na kufikia maamuzi ya kumleta kwenu kijana wetu Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza. Na pia mtajiuliza sasa kazi zitakuwa ila ataendelea kubaki kuwa Katibu Mkuu na tutaenda kwenye nginjanginja na ataoanga mipango ya namna gani ya kushinda.
“Pamoja nae pia tutaendelea kuwa na Dkt. Mpango kwa kuwa ndiye Makamu wetu wa Rais hadi pale tutakapomaliza naye,” alisema Rais Samia
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Mkutano Mkuu una mamlaka ya kufanya maamuzi hayo.Kulingana na Katiba ya CCM, Ibara ya 8(2)(a) inasema:-Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi una mamlaka ya kumteua mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Sehemu ya maelezo yaliyoko katika Azimio hilo yalikuwa yanasema hivi;”Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tukiwa tumekutana jijini Dodoma tarehe 18-19 Januari 2025, tunapitisha azimio hili kwa kauli moja:
Kumteua Mwenyekiti Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Hata hivyo kwa mujibu wa Katiba ya CCM*, Mkutano Mkuu una mamlaka ya kufanya maamuzi haya. Kulingana na Katiba ya CCM, Ibara ya 8(2)(a) inasema:-
“Hivyo Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi una mamlaka ya kumteua mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.”
WAHAFIDHINA Z’BAR
Kutokana na uamuzi huo wa Mkutano Mkuu wa CCM, inaelezwa kuwa awali kabla ya hatua hiyo kuna baadhi ya makada wa CCM Zanzibar walikuwa wameshaanza kupita huku na kule ikiwamo kuwaweka kwenye orodha ya malipo wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) kutoka Zanzibar kwa lengo la kutafuta kuungwa mkono.
“Ninachotaka kukumbia leo tumewakomesha watu ambao walikuwa na nia ya kutaka urais wa Zanzibar na sasa wamekwisha habari yao,”alisema Makame Juma
WALIOANZA KAMPENI
Awali akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Samia Suluhu Hassan alitoa onyo kali kwa watia nia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 walioanza kufanya kampeni za mapema kabla ya muda.
Kutokana na kauli taarifa kutoka ndani ya CCM iliambia Wamachinga kuwa kwa sasa makachero wa chama hicho wamemwagwa nchi nzima ili kufuilia nyendo za waotajw majimbo na kwenya kata mbalimbali kwa ajili ya kuwania ubunge na udiwani.
“Ninachotaka kukuambia kwamba kaika siku za hivi karibuni mtasikia kelele kubwa ambazo zitakuja kuleta utulivu wapo watu ambao wameanza kampeni za ubunge na udiwani na wanahangaika kila kona kutafutwa kuungwa mkono.
“Lakini ripoti za chama zinaonyesha kuwa makada wengi huenda wakajikuta wakiangukia kwenye adhabu hiyo na hata wengine kutoteuliwa na vikao vya chama kwa majina yao kukatwa,” alisema ofisa huyo ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini.