
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
– Asema mpaka sasa Marais wengi wamekwishafika
– Kufuatia uwepo wa ugeni huu Mkubwa baadhi ya barabara zitafungwa na kufunguliwa ili kuepusha usumbufu kwa wageni
– Asisitiza kuwa Serikali imeelekeza tarehe 27-28 Januari, 2025 Watumishi wa Umma Dsm kufanyia kazi Nyumbani
– Agusia suala la Usafi, Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila Leo tarehe 27 Januari, 2025 ametoa taarifa kwa Umma kupitia Waandishi wa Habari kuhusu Ujio wa Marais wanaotoka katika Mataifa ya Afrika kuhudhuria Mkutano wa Nishati tarehe 27-28 Januari, 2025 hapa Jijini Dar es Salaam
RC Chalamila amesema mpaka sasa Marais wengi kutoka Mataifa mbalimbali wamekwishafika aidha hoteli zenye hadhi kubwa zimekwishajaa na inaonyesha kuwa Rais Samia ameuandaa Mkutano huo kwa Viwango Vikubwa vya Kimataifa
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Ameeleza kuwa kufuatia kuwepo kwa ugeni huu Mkubwa baadhi ya barabara zitafungwa ili kuepusha usumbufu kwa wageni kama ilivyotangazwa na Jeshi la Polisi na msisitizo zaidi ni kuendelea kuvipunguza zaidi vyombo vya usafiri kupita kwenye zile njia ambazo zinaweza kuleta usumbufu Mkubwa kwa wageni wetu
Vile vile Mhe. Chalamila Amesisitiza kuwa *Serikali* imeelekeza tarehe 27-28 Januari 2025 Watumishi wa Umma Dar es Salaam kufanyia kazi Nyumbani isipokuwa wale ambao mazingira yao ya kazi yanawataka kuwepo katika Vituo vyao vya kazi kama vile Watumishi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Sekta ya Afya, Sekta ya Usafiri na Usafirishaji, Benki, Biashara Kariakoo, Hoteli na Migahawa aidhaa, Waajiri katika Sekta binafsi wanashauriwa kuruhusu Watumishi wao katika Mkoa wa Dar es Salaam kufanyia kazi Nyumbani au kuweka utaratibu ambao hautasababisha changamoto ya Usafiri kutokana na kufungwa kwa Barabara hizo
Mkuu wa Mkoa Amegusia Suala la Usafi kuwa unaendelea kufanyika katika maeneo yote na hali ya Ulinzi na Usalama ni nzuri kama taarifa ilivyotolewa na Jeshi la Polisi na Vyombo vya Dola hata hivyo baadhi ya njia Kuna magari mengi ya Polisi na Vyombo vya Dola hivyo kuwaasa wananchi wasiogope kwa sababu vyombo hivyo vinalenga kuhakikisha wageni pamoja na wenyeji wanakuwa *Salama* wakati wote
*Ikumbukwe kuwa Rais Samia anawatakia Watanzania wote na haswa wa Dar es Salaam kuendelea kuwa sehemu ya ukalimu kwa wageni wetu wanaokuja kuhudhuria Mkutano huo Mkubwa na utarushwa mubashara kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili Watanzani waweze kuelewa azma kubwa na heshima ambayo Taifa letu limepewa la kuwa mwenyeji wa mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na Marais wengi wa AFRIKA*