35 views 2 mins 0 comments

IRENE UWOYA AJA NA KAMPENI YA ‘JEMBE NI MAMA’ITAKAYOMKOMBOA MAMA KATIKA KILIMO CHA KIDIGITALI

In KITAIFA
January 27, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

MSANII Maarufu wa Bongo “Movie” Nchini Irene Uwoya ameanzisha kampeni ya kumkomboa mwanamke kwenye Sekta ya Kilimoa inayojulikana kama “Jemba ni Mama”.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 26, 2025 Wakati akitangaza kampeni hiyo Uwoya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mradi huo amesema asilimia 67 ya Wanawake ndiyo wanaojushughulisha na kilimo, hivyo ndiyo maana ameamua kuanzisha kampeni hiyo ili kuweza kuwasaidia kujikomboa kiuchumi.

“Mwanamke amekuwa akijuhusisha sana na Kilimo, lakini amekuwa akinyonywa kimaslahi, hivyo Mimi na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, tukaona tuje na kampeni hii ya Jembe ni Mama,” amesema Uwoya na kuongeza,

“Lengo la kampeni hii ni kuisaidia Wizara Kwa ajili ya kusimamia Mradi huu wa Kilimo kwa maslahi ya Mkulima Mwanamke. Hivyo kupitia Mradi huu tunataka kumkomboa mwanamke duni katika Kilimo,”.

Uwoya amebainisha kuwa kupitia Mradi huu wa Jembe ni Mama watatembelea Wanawake wakulima Nchi mzima ambapo ameeleza kuwa watapita mikoa yote ya Bara na visiwani Kwa kila Kata, Tarafa na Kijiji na kwamba watahakikisha wanawafikia Wanawake wakulima mashujaa kila Mwaka.

Kwamba kila Mkoa utatoa mwanamke Mkulima shujaa mmoja na hivyo kuwa na Wanawake mashujaa 26 Kwa mikoa yote.

Amebainisha kuwa wataanzisha tamasha kubwa kila Mwaka litakalojulikana kama Jemba ni Mama Festival ambalo litawakutanisha Wanawake wakulima pamoja na wadau mbalimbali watakaowasaidia kuendeleza Kilimo cha faida.

Uwoya ametumia fursa hiyo kueleza namna Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyoweza kufanya mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya Kilimo.

Kwamba Serikali imeweza kukifanya Kilimo kuwa cha kisasa, wakulima wanapata pembejeo za kisasa, wakulima wanatafutiwa Masoko ya ndani na nje na pia Kwa sasa Kuna Kilimo cha kidigitali.

Hivyo amesema kuwa Sekta ya Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi Kwa wananchi na Tanzania.

Kwa upande wake mshauri wa Rais Angellah Kairuki amempongeza Irene Uwoya kwa kuanzisha kampeni hiyo na kwamba imekuja Wakati mwafaka.

Ameeleza kuwa Serikali imafenya mageuzi makubwa Kwa ajili ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo ambapo Serikali imehakikisha kunakuwa na Sera na Mipango mizuri kuhakikisha Wanawake wanashiriki kwenye Kilimo.

Kadhalika imiweka Sera Bora na kuhakikisha kunakuwa na Mikopo kwenye Sekta ya Kilimo, elimu na Mafunzo kuhusu Kilimo yamekuwa yakitolewa Kwa wakulima pamoja na kuwatafutia Masoko ya ndani na nje.

/ Published posts: 1715

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram