24 views 19 secs 0 comments

WALIYOYAPAMBANIA WANAWAKE WENZETU MATUNDA YAKE TUNAYAONA – MBUJA

In KITAIFA
March 03, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

๐Ÿ“Œ *Asema Wizara ya Nishati inalo la kujivunia kutokana na uwepo wanawake katika nafasi za uongozi.*

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianoย  Serikalini Wizara ya Nishati,ย  Neema Mbuja amesema kile ambacho wanawake walikipambaniaย  katika majukwaa mbalimbali ikiwemo ya Kimataifa ili kuwa naย  haki, usawa na uwezeshaji kwa wanawake matunda yake yanaonekana hivi sasa.

Mbuja ameyasema hayo alipokuwa akieleza safari ya mwanamke katika kudai haki, usawa na uwezeshaji kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini kitaifa yatafanyika mkoani Arusha.

“Wanawake wengi walipambana kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia, usawa wa utendaji kazi na ushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na tangu kufanyika kwa Mkutano wa Beijingย  mwaka 1995 mambo yote ya usawa kwa sasa yanaonekana kwa vitendo.” Amesema Mbuja

Ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa kinara katika kuhakikisha haki kwa mwanamke inapatikana.

Ameongezaย  kuwa, Wizara ya Nishati inajivunia kwa uwepo wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.

/ Published posts: 1837

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram