
Na Madina Mohammed DODOMA WAMACHINGA

Katika mwaka wa fedha 2024/25 serikali inatarajia kupandisha vyeo watumishi laki mbili kumi na tisa na arobaini na mbili (219042)na kubadilisha kada watumishi elfu sita Mia tisa na kumi (6910).
Haya yameelezwa leo 3 march jijini Dodoma, waziri wa nchi ,ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora George Simbachawene katika kikao chake na wakuu wa Taasisi za umma.

Waziri Simbachawene ,amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili ya kazi kwani kumekuwa na malalamiko kuhusu vitendo vya uvunjifu wa maadili ikiwemo Rushwa, ulevi kazini ,matumizi ya lugha zisizofaa na kugushibarua za uhamisho.
Hata hivyo jukumu la waajiri wa watumishi wa umma ni kuendelea kuwasimamia watumishi waliochini yao kwa kuwa elimisha kuhusu haki na wajibu wao ili wanapodai haki wajue kuwa ni wajibu wanapaswa kutekeleza.
