61 views 2 mins 0 comments

TMDA IMEWATAHADHARISHA WAFANYABIASHARA WANAOINGIZA NA KUSAMBAZA DAWA NA VIFAA TIBA NA VITENGANISHI VIZIVYOSAJILIWA

In KITAIFA
April 04, 2025

Na Madina Mohammed WAMACHINGA

Ni muendelezo wa utoaji elimu kwa waingizaji na wasambazaji wa  dawa , vifaa tiba na vitenganishi  kutoka Wilaya ya Ilemela na Nyamagana Mkoani Mwanza ,Elimu hii inatolewa na mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki.

Mamlaka ya dawa na vifaa Tiba TMDA Kanda ya ziwa mashariki imewatahadharisha wafanyabiashara wanaoingiza na kusambaza dawa na vifaa Tiba na vitendanishi kutoingiza bidhaa ambazo hazijasajiliwa na mamlaka hiyo Ili kulinda afya za watumiaji

Ameyasema hayo 4 Machi 2025 wakati wakiwapa Mafunzo wafanyabiashara hao Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki  Sophia Mziray amesema bado wanaendelea na oparesheni mbalimbali ili kuhakikisha bidhaa hizo ambazo hazijasajiliwa haziwafikii watumiaji.

Amesema Ili kuleta dawa hizo ziwe salama na kuleta tija Kwa kile ambacho kinatarajiwa

Aidha amewaomba Rai wananchi kwamba wahakikishe wanaenda kwenye maduka ambayo mamlaka ya dawa na vifaa Tiba wamezisajili

Akifungua kikao kazi hicho Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Gabriel Mashauri akawataka wafanyabishara hao kuzingatia kanuni na sheria za uingizwaji wa vifaa hivyo.

“Kwa kuzingatia uingizaji wa Vifaa hivyo kwa wafanyabiashara Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria Ili huduma hii muhimu tunayotoa iweze kuokoa maisha ya wananchi Dunia”Amesema Mashauri

Baadhi ya waingizaji wa vifaa hivyo nao wakaiomba serikali kuendelea kudhibiti wimbi hilo.

Mfanyabiashara Mkoa wa Mwanza Derrickson Brigthony Amesema tukio lililofanyika nadhani kiwe kipaumbele Kwa wasimamizi wa mipaka,Kwa sababu mpakani wangekuwa hawaruhusu hata sisi huku tusingekuwa tunavipata

Mfanyabiashara Mkoa wa Mwanza Halima Mdoe Amesema sisi wafanyabiashara tunatumia pesa kuingiza hizo dawa alafu tunapozileta bidhaa kutoka nchini haionekani kwamba hazijasajiliwa Kwa hiyo tunakuwa tunatoa hivyo hivyo Kwa watumiaji Kwa kujificha au unakuwa madhara ambayo watakayoyapata Moja Kwa Moja watumiaji

/ Published posts: 2097

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram