38 views 55 secs 0 comments

WAKUU WA TAASISI ZA KIHABARI WAHUDHURIA UPITISHWAJI WA BAJETI YA WIZARA YA HABARI

In KITAIFA
May 07, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA



Taasisi mbalimbali za kihabari nchini zimepongeza uwasilishaji na upitishwaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, uliofanyika bungeni jijini Dodoma.

Bajeti hiyo imewasilishwa Mei 7, 2025 na Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Paramagamba Kabudi, akiambatana na Naibu Waziri, Mheshimiwa Hamisi Mwijuma, Katibu wa Wizara na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.



Wakuu wa taasisi hizo za habari waliohudhuria kikao hicho cha bunge, akiwemo Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura; Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile; Mwenyekiti wa MISA Tanzania (MISA-Tan), Edwin Soko,

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa OJADACT, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanahabari Kigamboni (KAJ) na Mratibu wa Kampeni ya Kaziinaongea Fatma Jalala, Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (JOWUTA), Caren-Tausi Mbowe, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya TEF, pamoja na Mhariri Mkuu mstaafu wa Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah

.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa MISA-Tan, Bw. Edwin Soko, ameeleza kuwa ongezeko la bajeti ni ishara ya dhamira ya Serikali katika kuimarisha sekta za habari, utamaduni na sanaa, ambazo ni nyenzo muhimu za kukuza demokrasia na utambulisho wa kitaifa.

Aidha, Soko ametoa wito kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzingatia uwezekano wa kuifanya sekta ya habari kuwa wizara huru, ili iweze kushughulikiwa kwa kina na kwa weledi, bila kuingiliwa na masuala kutoka sekta nyingine.

/ Published posts: 2097

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram