

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
๐บ_Makusanyo maduhuli yafikia asilimia 98 kwa mwaka 2024/2025_
๐*Ruvuma*
MAKUSANYOย ya maduhuli ya Serikali kupitia Sekta ya Madini katika Mkoa wa Ruvumaย yatokanayo na mrabaha, tozo na ada mbalimbali kwa mwaka wa fedhaย ulioanza Julai 2024/2025 ni Shilingi Bilioni 32.5.
Fedha hizo ni makusanyo ya mpaka tarehe 19 Mei, 2025 wakitarajiwa kuvuka lengo la fedha walilopangiwa la Shilingi Bilioni 33.15.

Akizungumza naย wanahabari wa Tume ya Madini, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi amesema, hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu Mkoa huo utakuwa umevuka lengo la zaidi yaย asilimiaย 100 ya ukusanyaji mapato.

Mhandisi Bikulamchi amesema kuwa mafanikio hayo yamepatikana kutokana na kushamiri kwa biashara ya makaa ya mawe ambayo kwa Mkoa wa Ruvuma yamebainika kuwa ni bora zaidi na yamekuwa yakiuzwa nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Bara la Asia na Bara la Ulaya.

Aidha, amesema pia Mkoa huo mbali na makaaย ya mawe pia umebarikiwa kuwa na aina nyingi za madini ikiwemo Dhahabu, Shaba,ย Chuma, Urani, Madini ya Ujenzi na Madini ya Vito.

Amesema pia kuna masoko mawili ya madini ambayo ni Soko la Madini Songea na Soko la Madini Tunduru ambayo yalianzishwa na Serikali kupitia Tume ya Madini ili kuongeza uwazi, usawa, ulinzi wa haki halali na maslahi ya watu wanaofanya biashara hiyo huku akiwataka watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo mkoani humo kama usambazaji wa teknolojia zinazotumika migodini, usambazaji wa bidhaa za vyakula, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini.
โ