14 views 3 mins 0 comments

NEEC YAZINDUA MWONGOZO WA KITAIFA KWA WATOA HUDUMA ZA MAENDELEO NA BIASHARA

In BIASHARA
May 21, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. JAMES KILABUKO ametoa wito kwa Jumuiya kuhakikisha kwamba inaimarisha na kufuatilia utendaji wa watoa huduma za maendeleo ya biashara Tanzania ili kusaidia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika kuratibu huduma za maendeleo ya biashara Tanzania.



Ameyasema hayo Leo 21 Mei 2025 Naibu katibu mkuu huyo wakati akimuakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi wakati akizindua Mwongozo wa Kiaifa kwa watoa Huduma za Maendeleo na Biashara.

Amesema Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ni kuimarisha utendaji wa masuala ya uwezeshaji ikiwemo huduma za maendeleo ya biashara ili kukuza shughuli za kiuchumi nchini.ย 

“Natambua kuna taasisi mwamvuli ya watoa huduma za maendeleo ya biashara Tanzania ambayo inaitwa: Jumuiya ya Watoa Huduma za Maendeleo ya Biashara Tanzania”. Amesema Kilabuko



Aidha Kilabuko Amesema Serikali ilianza kusimamia masuala ya uwezeshaji kiuchumi tangu Tanzania ilipopata Uhuru ambapo mwaka 2004, Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ilitungwa. Uwezeshaji kiuchumi ni dhana inayobeba dira ya nchi inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Pia Amebainisha kuwa Dhana ya uwezeshaji kiuchumi kama inavyobainishwa katika Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi, ni dhana mtambuka inayotekelezwa na sekta zote nchini ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu ikibeba jukumu mama la kuratibu utekelezaji wake.

Aidha Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa Amesema kuwa kwa Muda mrefu wafanyabiashara Wetu wamekuwa hawapati misaada ya ushauri wa jinsi ya kuendeleza biashara zao kwahiyo mwongozo utasaidia sana kwa wale ambao wanawasaidia wafanyabiashara katika kazi zao.

Beng’i Issa Amesema kuwa mwongozo huo umezingatia kwamba unapomsaidia mfanyabiashara kumpa ushauri au kumsaidia katika ushauri wa kitaalamu lazima kuwe na matokeo.

“Huwezi kumsaidia mtu labda anakulipa pesa baada ya pale hakuna mabadiliko Katika biashara yake na vitu hivyo vimezingatiwa na kujifanyia assessment kwa huyo mfanyabiashara kwa kuangalia kama amepiga hatua na wakati unamsaidia uwe na kipindi ha kumsaidia na kuonekane kama Kunka mwisho wa kumsaidia”. Amebainisha Issa

Nae Mkurugenzi mkazi wa MEDA Mussa Lugambo Amesema kuwa mwongozo huo utawasaidia sana watoa huduma kuweza kuwasaidia watoa huduma ambayo itawasaidia wajawasiriamali kwa ajili ya kutekeleza biashara zao.



“Tumekuwa na changamoto kwa watoa huduma ambapo unakuta kwamba huduma ambayo inayotolewa kwa wajawasiriamali inakuwa siyo ya kiwango kizuri na hivyo kushindwa kuwasaidia wajawasiriamali kuendeleza biashara zao” Amesema Lugambo



Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Chambers Bi. Mwajuma Amesema mwongozo huo ni mzuri sana hasa kwa wale wanaofanya kazi na wajawasiriamaliย  wote Katika Sekta zote nchini tutawaongoza watu wote ambao wanaotoa huduma hizi Kwa maendeleo ya biashara nchini.

/ Published posts: 2085

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram