
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ambaye pia ni mwanachama wa klabu ya Simba Mhe. Ussi Salum Pondeza asisitiza kuwa komba la Shirikisho barani Afrika ni lazima litwaliwe na vigogo wa soka nchini Simba SC.
“Lazima kombe tubebe, nasema tena lazima kombe tubebe lakini hatutashinda kama hatutakuwa kitu kimoja, kila Mwanasimba ana mchango katika Simba yetu, sio lazima kitu kikubwa.” Amesema
Aidha mwanachama huyo amewahimiza wanachama,mashabiki na wapenzi wa klabu ya simba kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili ya May 25, 2025 kwenye fainadi hiyo ili waweze kumlaza Mmorocco.
“Siku ya tarehe 25 twende uwanjani mapema na kushangilia muda wote. Deni kubwa ambalo tupo nalo ni kumheshimisha mtoto wa Hayati Rais Mwinyi ambaye ni Rais wa sasa Dkt. Hussein Mwinyi. Na kumheshimisha ni kumpa kombe.” ameongeza
Simba SC itacheza fainali hiyo Dhidi ya RS Berkane ya nchini Morocco katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar