21 views 2 mins 0 comments

CHALAMILA, SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

In KITAIFA
May 23, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wauguzi nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kufuata misingi ya sheria ya kazi yao ili kulinda afya za wananchi na kwamba Serikali Mkoani humo inatambua na kuthamini kazi ya uuguzi katika kulinda afya za wananchi

Akizungumza leo Mei 23,2025 Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya wauguzi kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema wauguzi ni nguzo muhimu kwenye utoaji wa huduma za afya hivyo ni muhimu kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu kama ambavyo kanuni za kazi hiyo zinavyowataka

Aidha RC Chalamila ameitaka jamii kutambua na kuthamini kazi inayofanywa na wauguzi na kusisitiza kuwa Serikali Mkoani humo itaendelea kushirikiana na wizara ya afya ili kuimarisha zaidi mazingira ya utolewaji wa huduma za afya, pia akiisisitiza jamii kuendelea kutambua sera ya afya inayohitaji wananchi kuchangia huduma hiyo

Sanjari na hayo amesisitiza wakazi wa jiji hilo na watanzania kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa mujibu sheria kwani kodi ndio nyenzo ya kuboresha huduma za kijamii ikiwemo  huduma za afya na amemshukuru Rais Dokta Samia kwa namna ambavyo amekuwa akiimarisha upatikanaji wa huduma za Afya hivyo amesisitiza kuwa wauguzi ndiyo faraja kubwa kwa wagonjwa

Kwa upande wake Rais wa chama cha Wauguzi Tanzania Tanna Ezekiel Henry amewataka wauguzi kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kufuata sheria na kanuni za kazi hiyo huku akiitaka jamii kuheshimu kazi ya uuguzi kwenye kulinda afya za wananchi

Kwa upande wake Rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA Dokta Beatrice Mwilike amezungumzia umuhimu wa ushiriki wa wanaume kwenye Afya ya mama mjamzito wakati wa kujifungua na kwamba wanaendelea kuimarisha mafunzo kwa wakunga ili kuboresha huduma huku Kaleb Kiula Muuguzi kutoka hospitali ya Mloganzila wakati akisoma risala ameiomba Serikali kudhibiti kazi za baadhi ya wasanii wanaodhihaki kazi ya uuguzi.

Maadhimisho hayo yamebeba kaulimbiu isemayo “Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko Duniani”ambapo kupitia maadhimisho hayo wauguzi wamewasha mshumaa wa upendo na kula kiapo cha kufanyakazi kwa uadilifu na kutunza siri mbele ya mkuu wa Mkoa

/ Published posts: 2101

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram