
Dodoma
Imeelezwa kwamba Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imekuwa na mchango mkubwa katika serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwasilisha mada katika Mkutano wa Maafisa habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TARURA,Mratibu wa Mradi wa Agri-Connect Mhandisi Claver Mwinuka amesema serikali ya Awamu ya Sita imeongeza bajeti ya TARURA mara tatu zaidi ili kuhakikisha barabara za vijijini zinapitika kwa misimu yote.
“Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza bajeti ya TARURA mara tatu zaidi lengo ni kufikia asilimia 85 katika ujenzi na matengenezo ya barabara nchini.
Amesema mchango huo wa TARURA umeweza kuleta mafanikio makubwa ikiwemo uboreshaji wa barabara, ujenzi wa madaraja na miundombinu ya maji, ujenzi wa barabara za changarawe,matumizi ya teknolojia mpya ambapo barabara hizo zimeweza kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara kufikia masoko.