14 views 3 mins 0 comments

BALOZI WA SWEDEN MHE.CHARLOTTA MACIAS: UCHUMI WA BLUU SERIKALI WANALIANGALIA KWA UMAKINI SANA

In BIASHARA
May 29, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias Amewataka wajawasiriamali wa kilimo Cha mwani kuwa waende wakazungumze na waanzilishi wa miradi.ili kutazama walichokijenga. na Kuwa na shauku ya kupata Suluhisho ambalo linalofuata la kubadili mchezo kuhusu taka baharini au uendelevu wa bahari.



Ameyasema hayo Leo 29 Mei 2025 Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe.Charlotta Ozaki Macias Amesema kuwa mila ya Nordic ya uendelevu na ubunifuโ€”ambayo imejikita sana katika tamaduni zetu. Nchi za Nordic zimekuwa mstari wa mbele kwa muda mrefu katika biashara inayowajibika, uongozi wa kimazingira, na suluhisho za kisasa. Hivyo basi ni jambo la busara kuleta roho hiyo hapa, tukisaidia juhudi za ndani na za kimataifa kulinda sayari yetu ya pamoja.



Ameongeza kuwa uhusiano wa Nordic ni imara, kupitia wadau wa Nordic kama TechBridge na MTI, ambao wanaendesha programu ya Elevate Blue.
Basi, na tuhakikishe leo ina maana. Tuwapongeze hawa wabunifu. Tuunde mitandao. Na pia nawakaribisha kila mmoja wetu kutafakari kuhusu tabia zetu binafsi. Iwe ni kuacha kutumia chupa za plastiki kwenye matukio yenu au kushiriki katika usafi wa fukweโ€”kila mmoja wetu anaweza kufanya jambo kuhakikisha bahari zinadumu kwa vizazi vijavyo.



“wawekezaji, wawakilishi wa serikali, na wadau: Hampo hapa kushangaa tu. Mko hapa kushiriki. Kuuliza maswali, kuhoji mawazo, na kushirikiana. Mustakabali wa maendeleo endelevu utajengwa juu ya ushirikiano unaounganisha mawazo bora na rasilimali zinazohitajika kuyatekeleza”. Amesema Macias


Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt. Amos Nungu Amesema kuwa Katika uchumi wa bluu ni eneo ambalo serikali wanaloliangalia Kwa umakini sana.”Tunawashukuru hawa wezetu Kwa kuja na hii programu”



Ameongeza kuwa ukiangalia Katika zao la mwani serikali Kupitia costech wamekuwa wakisaporti Kwa Muda mrefu kule Zanzibar ameonesha mfano kuwa mwaka juzi tuliwanunulia viboti vile vidogo Kwa ajili ya maswala ya mwani kwenye eneo ambalo tunalifanyia kazi.

“Wakati mwingine changamoto iliyopo kwamba huwatuna Ubunifu wa teknolojia peke. Yake wakati mwingine watu wanashea Ubunifu na maswala mengine”Amesema Nungu



Pia Mkufuzi wa maswala ya mwani Farhiya Elmy Amesema zao la mwani linamambo.mengi linaweza kutengeneza prasitiki Kupitia mwani sio tu sabuni unaweza kutengeneza pafyumu

Amesema vijanaย  Wengi wamekuwa wakifanya Vitu Kwa urahisi vitu ambavyo wanajua wakifanya Leo kesho vitaingia sokoni hawako tayali kukaa chini Kwa kufanya research ya kujifunza Kwa kuleta kitu ambacho kitaleta manufaa na mabadiliko Katika nchi yetu



Aidha amewaomba serikali kuwa Sera zilizopo hazikidhi mahitaji Kwa mkulima wa mwani pia mfanyabiashara mdogo wa mwani sera waziboreshe “tukija watanzania bara hatuna sera ambayo inayouhusiana Moja Kwa Moja na uchumi wa bluu sera zitakazotengenezwa zitengenezwe Kwa mujibu ya mahitaji Kwa wafanyabiashara pamoja na wakulima Ilikuweza Kuendeleza system bilt”. Amesema Elmy

/ Published posts: 2133

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram