28 views 8 secs 0 comments

ILANI YA CCM MSINGI WA FIKRA MPYA KWENYE UCHUMI WA TANZANIA – DKT. KAHYOZA

In KITAIFA
May 31, 2025



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Mei 30, 2025, amezindua Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2025/2030, jijini Dodoma, katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama.

Ilani hiyo mpya inalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa vipaumbele tisa ikiwemo uchumi, sayansi na teknolojia, miundombinu, na utawala bora.
Dkt. Kahyoza, mchumi, amesema Ilani hii ni fursa ya kupima kwa vitendo falsafa ya “Samia-nomics”, akieleza kuwa inajibu changamoto za umaskini kwa kupeleka maendeleo hadi ngazi ya wananchi.

“Ni Ilani ambayo inajaribu kufanya ugatuaji wa mitaji kutoka Serikali Kuu kwenda kwenye Serikali za Mitaa, ukiangalia fursa zinarudi kule chini kwa watu” amesema.

Kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025/2030, Dkt. Kahyoza amesema Taifa linaweza kufikia ile dhana ya kubadilisha rasilimali zetu za asili tulizonazo kuwa rasilimali za kiuchumi.

/ Published posts: 2141

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram