19 views 26 secs 0 comments

RC SERUKAMBA AITAKA  TRA KUDHIBITI RISITI FEKI, KUHAMASISHA ELIMU YA KODI

In KITAIFA
May 19, 2025



‎Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Peter Serukamba, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo kuhakikisha wanadhibiti utoaji wa risiti feki kwa bidhaa mbalimbali, akisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFD) ili kuongeza mapato ya serikali.

‎Akizungumza leo Mei 19, 2025 ofisini kwake baada ya kupokea ugeni wa Viongozi kutoka TRA Makao makuu uliofika kwa ajili ya kuanza kampeni ya utoaji elimu kwa mlipakodi kwa njia ya “Mlango kwa Mlango”, Serukamba alisema kuwa ni muhimu kwa maofisa wa TRA kutumia elimu na si nguvu wakati wa kukusanya kodi.

‎Aidha, Mhe Serukamba amewahimiza wafanyabiashara wote mkoani Iringa kupokea elimu hiyo kutoka kwa wataalamu wa TRA na si kufunga maduka au kuwaogopa.

‎Sambamba na hilo kampeni ya “Mlango kwa Mlango” inalenga kuelimisha wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari, matumizi sahihi ya mashine za EFD, na kutoa risiti kwa kila mauzo.

‎”Ni muhimu kwa kila mfanyabiashara kutoa risiti halali kwa kila mauzo na kulipa kodi stahiki na hii itasaidia serikali kupata mapato ya kutekeleza miradi ya maendeleo,”amesema Serukamba

/ Published posts: 2083

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram