16 views 42 secs 0 comments

MFUMO MPYA WA KIDIGITALI WA KITAMBULISHO KUANZA RASMI

In KITAIFA
May 19, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

MWENYEKITI wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ,Tido Mhando ametangaza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa kidijitali wa kupata Ithibati ya Kitambulingo Cha Uandishi wa Habari (Press Card ) kupitia. Mfumo wa https://www.taihabari.jab.go.tz


‎Hayo yamebainishwa Leo Mei 19,2025 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti huyo amefafanua kwa kusema kuwa waandishi wanatakiwa kuwa na vitumuhimu kamaPicha ndogo(passport size),vyeti vya elimu,Kitambulisho Cha Taifa(NIDA),Barua ya utambulisho kutoka taasisi au anakopeleka kazi zake ikiwa ni mwandishi wa kujitegemea (Freelancer) na Ada ya Ithibati shilingi Elfu Hamsini(50,000).

‎Aidha,ameeleza kwamba baada ya kuwasilisha maombi mwombaji atapokea ujumbe wa SMS kuonyesha hatua ya maombi yake kama yanashughulikiwa,Amekubaliwa,Yamerudishwa kwa marekebisho au Yamekataliwa.

‎Pia amesema kama maombi yatakubaliwa,Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari itamjulisha mwombaji mahali na muda wa kuchukua Kitambulisho(Press Card) na kitambulisho hicho kitatumia sehemu yoyote ya kihabari ndani na nje ya taasisi.

‎Aliendelea kwa kusema kwamba hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17@ ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari ,inalenga Wahariri,Waandishi wa Kujitegemea(Freelancers na Correspondents),Watangazaji,Wapiga pocha,Waandaaji wa vipindi vya habari(Producers),Wanafunzi wa Vyuo vya Uandishi wa habari na Waandishi wa habari wa kigeni.

/ Published posts: 2080

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram