







Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Taasisi ya Flaviana matata Kwa kushirikiana na kufadhiliwa chini ya Shirika la WFT ambao ni wadau wakubwa wa kuhakikisha wanalenga jamii na Lengo kubwa ni kuweza kuwawezesha waandishi wa habari kuwaongezea ujuzi kuhusiana na mada ambazo zinawafanya wanapofanya kazi iwe rahisi kupata taarifa ambazo ni sahihi Ili zisiweze kupotosha jamii
Taasisi hiyo imetoa semina Kwa waandishi wa habari Katika Lengo la kuwapatia Mafunzo ya afya ya uzazi pamoja na ukatili wa kijinsia
Ameyasema hayo Leo 22 Mei 2025 Afisa Miradi Flaviana matata Foundation Suzan Cleophas Ambapo Alipokuwa wanatoa Mafunzo Kwa waandishi wa habari Katika ofisi za Flavian matata Foundation jijini Dar es salaam
Amesema kuwa Tunaamini kwamba media zinafanya kazi kubwa sana Kwa hiyo elimu hii itasaidia kufikisha ujumbe Kwa jamii Zaidi na Zaidi
Aidha Amesema kuwa Mradi huo umeweza kutolewa Tokea Mwaka Jana walianza na wanafunzi na kufuatia Kwa waandishi wa habari
“Mradi huu hatujaaza na waandishi wa habari hapo awali uliaza mwaka Jana tulianza na wanafunzi tulienda Katika mkoa wa pwani tulikutana na wanafunzi 200 wa shule ya kiwango na msata na baadae tulifata media na kupita baadhi ya media na tukaona kunauhitaji mkubwa wa kukusanyisha media mbalimbali na kuweza kuwapatia taarifa, mradi huu umefanyika Kwa namna mbalimbali na hatujafanya Kwa media pekee na tumefanya na CHW”Amesema Cleophas
Cleophas Amebainisha kuwa wanafanya Kazi na serikali na kutambulika na wizara ya afya,wizara ya elimu lakini pia hakuna kitu chochote kinachotoka ambacho kipo chini ya serikali, Amefafanua kuwa “EGo yetu imesajiliwa na serikali na inatambua na hata Kwa ngazi ya chini tunafanya kazi mkoa wa shinyanga,Njombe,Pwani,Ruvuma na mwanza Kwa hiyo juu tunatambulika lakini chini tunafanya kazi na halmashauri na Vitongoji vyake”.
Amesema Kwa mikoa ambayo waliyowai kufanya nao kazi wameichagua kutokana na takwimu za serikali na kuangalia umuhimu wa elimu Kwa Mikoa hiyo
“lakini pia Katika matukio haya ya kikatili yako vipi Katika mikoa hiyo elimu Bado tunaendelea kuitoa kutokana na mpango Wetu wa mkakati wa miaka 5 matukio yanapungua lakini elimu Bado inaitajika Kwa sababu”.
Nae Rehema longo ni mwezeshaji wa Mafunzo ya stadi za maisha kitaifa Amesema kuwa tunashukuru Kwa Flaviana matata Kwa kutambua umuhimu wa kuisaidia serikali Katika kuielimisha watu Ili waweze kufahamu stadi za maisha Kwa sababu stadi za maisha ni muhimu sana Kwa kila mmoja Wetu Kwa jamii zetu tunazoishi
“Leo hii tumekutana na waandishi wa habari wameweza kujifunza mambo mengi Kuhusu jinsi ya jinsia na kuangalia Kuhusu afya ya uzazi lakini unawezekana siku nyingine anaweza kupata nafasi akawaita kupata elimu Zaidi kuhusiana na mambo ya stadi za maisha”Amesema Longo
Ameongeza kuwa Hizi stadi za maisha tunazoziongelea Kwa mana ya kwamba vinaweza kusaidia sana vijana hata kama ni mtu mzima au jamii yoyote Ile inaitaji