
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Baadhi ya Wanaharakati nchini Tanzania wametoa rai kwa vijana wa kenya ambao wanaendelea kumkebehi na kumtukana Rais DKt Samia suluhu Hassani na kuchochea vurugu na Vitendo vya uchochezi nchini.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mwanaharakati Ahmedi kombo mara baada ya kuzungumza na Wanahabari ambapo ametoa rai kwa baadhi ya vijana kutoka kenya kuacha kufanya Vitendo vya uchochezi nchini kwetu Tanzania kwani wanaharibu sifa za nchi yetu na viongozi kwa ujumla wakati huku Rais huyo huyo anaendelea kujenga Maendeleo mbambali ya nchi katika kujikwamua kiuchumi.
“Sisi kama vijana wazalendo tumeona tutoe tamko kwa kile kinachoendelea Tanzania hatutokubali mtu yeyote aweze kuvuruga na kuharibu amani ya nchi yetu pia kuna mwanasiasa kutoka kenya Martha karua naye anaungana na baadhi ya watanzania kusema baadhi ya viongozi wetu aendelee na shughuli nyingine nchini kwake atuachie nchi yetu. “Amesema kombo”
Aidha tutaendelea kukemea Vitendo hivi katika kipindi hiki tunachoenda kwenye uchaguzi mkuu hivyo kwa sasa nchi yetu iko salama katika Vitendo hivyo vya uhalifu huku jeshi la polisi likiendelea kulinda Ulinzi na usalama wa Raia.
Vilevile Kuna Mitandao ya kijamii inatumia kupotosha watu pasipo na ukweli wowote na kutoa taarifa ambazo sio sahihi hivyo kwani viongozi wetu wanajitahidi kulinda Wananchi wake nyakati zake
Mwanaharakati wa siasa Joseph Yona Amesema kuwa kuna chama pinzani bado kinaendelea na uchochezi wa kisiasa kwa kutumia watu kadhaa na kuharibu sifa za viongozi wetu nchini sisi kama wanaharakati hatutokubali kuwachafua viongozi wetu kwa namna yeyote ile tutaendelea kukemea vikali.
Nchi yetu ina Amani hivyo kuna Watu wachache akiwemo Maria Sarungi na kundi lake kutaka kuifanya Tanzania Sehemu ya vita tunatoa wito kuwa Nchi yetu haihitaji vita wala mapigano tunahitaji Amani tu sio vinginevyo “Amesema Joseph Yona”