KATIBU MKUU MKOMI AZISISITIZA TAASISI ZA UMMA KUSHIRIKI KIKAMILIFU WIKI YA UTUMISHI WA UMMA; AWAALIKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATA HUDUMA
Na Mwandishi wetu-Dodoma. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amezisisitiza Taasisi za Umma zilizoalikwa kushiriki Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kushiriki kikamilifu maonesho hayo yatakayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2025 ili wananchi waweze kupata huduma za papo kwa […]