

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
KATIBU Mkuu Wizara ya Madini Eng. Yahya Samamba amesema kutokana na utulivu uliopo katika sekta ya madini , amekishauri Chama Chama cha Watoa Huduma Migodini (TAMISA), kunoa makucha yake ili kidhibiti wanachama wake wasio waaminifu katika utoaji huduma.
Ameyasema hayo Leo 16 Mei 2025 Katibu Mkuu wizara ya madini Eng.Yahya Samamba wakati akizindua kamati ya masoko na mawasiliano na kamati ya utetezi pamoja na Ubunifu jijini dar es salaam
Amesema kumekuwa na malalamiko kama serikali baadhi yenu wamekuwa sio waaminifu na wanaleta ujanja ujanja na kusambaza bidhaa ambazo hazina kwaliti
“mtu anavyokuwa ameweka pesa yake na wewe Unavyoleta ujanja ujanja wako wa mtaani Katika
kazi yake Kama serikali hatutovumilia”Amesema Samamba

Pia Amesema Ifanyeni TAMISA kama ilivyokuwa IRB,”mtu akicheza na enginia akicheza na IRB inamuaibisha embu ifanyeni iwe na ukubwa huo,mukifanya muwe na ukubwa huo mutafanya kuwa na wasambazaji wenye nidhamu ,wenye kujitambua,na hawaiangushi nchi Kwa kile ambacho munachokipush”.
Aidha amewataka TAMISA wawe na ushirikiano na wizara na taasisi zake ambazo zitatoa ushirikiano Kwa asilimia 100 ambayo ni maelekezo ya Mhe Rais Samia kwamba watanzania na taasisi za kitanzania kuweza kuwapa ushirikiano Kwa asilimia 100 kwanza,haimaanishi kwamba hatuwakalibisha wawekezaji kutoka nje na haimaanishi hatuwapi ushirikiano kutoka nje tunafanya hivyo Kwa usawa
Aidha Ameelezea kuwa TAMISA ni changa inaitaji members naamini Kuna katiba na Kuna utaratibu wa kupata members musiwe kama vyama vingine ambavyo sivitaki kuvitaja, kwenye majukwaa wanakuwa wengi sana tunashabikiana kama tupo pamoja
“Kunakuwa na chama ambacho hakina nguvu hakikisheni zile hatua zote za kufata kuwa Wanachama wa TAMISA zote tumezitekeleza kama Kuna Ada tulipe ada Ili kusudi chama kiweze kujiendesha najua tumepata mwenyekiti mzuri tunaweza kuunda mifumo mingine kupata source of fund na kulani organisation lakini najua ada nimoja wapo ya vyanzo hivyo tuwe na chama chenye watu hai wenye kujitambua
Pia Amesema TAMISA ni miongoni mwaazima ya serikali ya awamu ya Sita ambayo Sekta ya madini inachangia ipasavyo Katika Pato la Taifa ikilinganishwa na Sekta nyingine za uchumi za kuleta maendeleo

Tusiishie kusambaza, tujenge Viwanda vya ndani kwenye takwimu ya serikali,Twendeni tukajenge.viwanda Ili kusudi tusiwe law source of material kwenda kwenye nchi zingine kuomba ajira na varue change ya madini
Hakikisheni TAMISA imekua na kupata kazi na kufanya kazi ya watanzania Kwa manufaa ya nchi yetu na kuwataka pindi wanapoingia Katika ofisi ya serikali kwenda kuongea Kuhusu maslahi ya watanzania kwa kujiendesha Katika migodi
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Dr Sebastian Ndege amewashukuru wanachama na wageni waalikwa kwa kushiriki kwenye uzinduzi huo ambao uliambatana na mipango ya mikakati ya TAMISA na Wizara ya madini nchini.
Dr. Sebastian Ndege amesisitiza Kwa kusema kuwa “siku ya leo sio siku tu muhimu kwa TAMISA kwa uzinduzi wa kamati yetu, bali pia ni mwanzo mzuri wa mapinduzi makubwa yanayoenda kutokea kwenye ushiriki wa wazawa na Watanzania kwenye uchumi wa sekta ya madini”