
Na Mwandishi Wetu NORWAY
IMEELEZWA kuwa Bandari ni chanzo kingine Cha biashara ya kaboni ambapo Ingvar M. Mathisen, Mkurugenzi mkuu wa Bandari ya Oslo, Norway ameyasema haya kwa ujumbe wa Tanzania uliotembelea bandari Nchini humo hivi karibuni.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mha. Masauni, ulitembelea bandari hiyo kwa lengo la kujifunza namna Bandari ya Oslo inahifadhi mazingira na kuzuia uzalishaji wa gesi joto.
Akizungumza , Mkurugenzi mkuu wa Bandari hiyo Mathisen ameeleza kuwa Bandari ya Oslo ni bandari mtambuka na haizalishi gesi joto. Bandari ya Oslo ni bandari ya tatu kwa ukubwa duniani kwa kuwa na teknolojia janja ya bahari.
Lengo kuu la bandari hiyo ni kuhakikisha kuwa inapunguza jesi joto kwa 85% ifikapo mwaka 2030.
Serikali hiyo imeazimia kufikia lengo hilo kwa kutumia teknolojia.
Kuanzia mwaka 2018 Bandari ya Oslo, Norway imeacha kupokea na kuendesha meli zake kwa kutumia mafuta, badala yake meli zao iwe za kisafirisha abiria, mizigo au starehe zote zinatumia umeme.
Hivyo kwa vyombo vyote ambavyo havitumii teknolojia hiyo, bandari ya Oslo hutoza ada ya uzalishaji gesi joto-โ Emission Feesโ( inayo jumishwa kwenye mpango wa biashara ya Kaboni).
Tanzania ni nchi ambayo Mashariki yake ina pwani ndefu ya bahari ya Hindi ambayo ina bandari kubwa ya Dar Es Salaam, Mtwara na Tanga aidha kuna bandari ndogo zinazohudumia Lindi, Kilwa Masoko, Mafia, Pangani na Kwale.
Bandari zote hizi hutumia vyombo vya usafirishaji. Hivyo kwa kuwa na teknolojia ya kutambua kila chombo huzalisha kiasi gani cha gesi joto, Mamlaka husika kwa kushirikiana na Kituo cha Ufuatiliaji wa Kaboni – NCMC zinaweza kufanya biashara hiyo kwa kudai ada ya uzalishaji gesi joto.
Kupitia ziara hiyo Tanzania imebainisha fursa mbalimbali za uhifadhi na usimamizi wa Mazingira kupitia Uchumi wa Buluu na Biashara ya Kaboni.