12 views 2 mins 0 comments

WAZIRI MKUU MAJALIWA ACHAGIZA SIKU YA TANZANIA  MAONESHO YA  EXPO 2025, JAPAN

In KITAIFA, Uncategorized
May 25, 2025



📌 *Asema Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji kwenye Jotoardhi, Kilimo, Uchumi wa Buluu, na Utalii*

📌 *Anadi Maonesho ya Sabasaba nchini Japan*

📌 *Japan yasifu ukuaji wa uchumi Tanzania; Yaahidi kuendeleza ushirikiano*

📌 *Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu washiriki siku ya Tanzania Japan*

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la biashara kati ya Tanzania na Japan kutoka dola za kimarekani bilioni 7 mwaka 2020, hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 37 mwaka 2024 na hivyo kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye nyanja za kiuchumi.

Mhe Majaliwa ameyasema hayo leo 25 Mei, 2025 jijini Osaka  Japan wakati akimwakilisha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya Siku ya Tanzania kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025 yanayoendelea nchini Japan,ambapo amesema Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji  kwenye miradi ya Jotoardhi, Uchumi wa buluu, Afya, Elimu, Miundombinu, Kilimo, na Mifugo.

Aidha Mhe Majaliwa ametumia fursa ya siku ya Tanzania kuyaalika kampuni za Japan kuwekeza nchini pamoja na kushiriki kwenye maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama sabasaba ambayo hufanyika kuanzia  mwishoni mwa mwezi  juni.

‘’ Nipende kuwakaribisha wenzetu wa Japan kuja kuwekeza Tanzania kwani mazingira ya uwekezaji ni mazuri ‘’ Amesema Mhe Majaliwa

Siku ya Tanzania kwenye maonesho ya Osaka Expo 2025 nchini Japan ilipambwa na ngoma za utamaduni na Taarabu asilia kutoka Zanzibar na kuhudhuriwa pia na Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi mbalimbali sambamba na maonesho ya Wiki ya Miundombinu  ya Osaka Expo 2025  yanayoendelea nchini Japan.

/ Published posts: 2108

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram