24 views 2 mins 0 comments

ULEGA AMBANA MKANDARASI BARABARA KUELEKEA MAKAO MAKUU YA JESHI (JWTZ).

In KITAIFA
June 01, 2025



๐Ÿ“Œ Amtaka akabidhi barabara ifikapo Disemba mwaka huu

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemtaka Mkandarasi Kampuni ya CHICO kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kikombo โ€“ Chololo – Mapinduzi (Makao Makuu ya  Jeshi la Kujenga Ulinzi la Wananchi-TPDF) yenye urefu wa kilometa 16.4 kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Disemba, 2025.

Ulega ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma leo Juni 01, 2025 akiwa ameongozana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax na kukagua barabara hiyo ambayo utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwa sababu ya upungufu wa wafanyakazi na mitambo ya ujenzi.

โ€œTumekagua barabara hii, Sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wake sasa nitoe maelekezo mahususi kwa barabara hii, Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana, aongeze vifaa na mitambo ya ujenzi lakini pia azalishe ajira kwa wakazi wa maeneo haya ili barabara hii ikamilike kwa viwango na muda tuliompa kimkatabaโ€, amesisitiza Ulega.

Waziri Ulega amemuagiza Mkandarasi CHICO kuhakikisha anaboresha mpango kazi wake ili aweze kukamilisha kazi zilizobakia zikiwemo ujenzi wa makalvati pamoja na madaraja katika barabara hiyo.

Aidha, Waziri Ulega amebainisha kuwa Serikali hivi sasa ipo katika hatua za mwisho za manunuzi za kumpata Mkandarasi wa kujenga barabara ya njia nne na sita kuanzia Chamwino Ikulu hadi katikati ya jiji la Dodoma.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax ameeleza kuwa ni matumaini yake ujenzi wa barabara hiyo utakamilika kwa muda uliopangwa na ikiwa na ubora na viwango vinavyotakiwa.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj. Jabir Shekimweri amewashukuru Mawaziri hao kwa kufika na kukagua hatua za barabara hiyo  kwani lengo la barabara hiyo ni kuleta muunganiko na ukaribu kati ya Wilaya za Dodoma Mjini na Chamwino hivyo utachochea maendeleo katika maeneo husika.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Japherson Nnko amewahakikishia Mawaziri hao
kuusimamia kwa karibu utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa muda uliopangwa ambapo hadi sasa umefikia asilimia 51.

/ Published posts: 2144

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram