
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar ea Salaam imefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa miradi mbalombali ya maendeleo Wilaya ya Kigamboni ikiwa ni katika kutazama utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2020/2025 ambapoย imeeleza kuridhishwa na utekelezaji huo.
Kamati hiyo imeongozwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bwana Elias Mpanda aliemwakilisha Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo wakiambatana na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Albert Chalamila ambaye ndiye msimamizi mkuu wa utekelezaji wa ilani kwenye Mkoa huo.
Akizungumza katika ziara hiyo Wilayani kigamboni jijini Dar es salaamย Mkuu wa Mkoa Mheย Albert Chalamila amesema katika utekelezaji wa ilani kwenye ujenzi wa shule na vituo vya afya kwa sasa Mkoa umeweka utaratibu wa miradi hiyo ya vituo vya afya na shule kujengwa kwa mfumo wa ghorofa ili kuepuka changamoto ya uhaba wa Ardhi lakini pia matumizi bora ya Ardhi kwa kuwa watu wanazidi kuongezeka Ardhi bado ni ileile.
Aidha akiwa kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mkoa inayojengwa Kigamboni RC Chalamila amesema mpango wa kuwa na shule za Mkoa ikiwemo ile ya wasichana iliopo kwembe wilayani Ubungo ni kuwa na mfumo wa elimu utakaowezesha watoto kupata elimu za ufundi na stadi za maisha baada ya kumaliza shule
Aidha pamoja na kamati hiyo kuonesha kuridhishwa na kazi ya utekelezaji wa ilani ya CCM RC Chalamila amewasisitiza wakandarasi kutumia vyema fedha inayotolewa na Rais Dkt Samia kwa kuelekeza fedha hizo kwenye miradi husika na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia thamani ya fedha na viwango stahiki.
Kwa upande wa Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bwana Elias Mpanda akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa kwenye ziara hiyo amesema chama kimeridhishwa na utekelezaji wa ilani kwenye wilaya hiyo na kusisitiza miradi ikamilike kwa wakati na kwa Viwango stahiki.
Katika ziara hiyo kamati ya siasa ya CCM ya Mkoa imetembelea shule ya Sekondari vumilia ukooni iliyoko Kata ya kisarawe two, ujenzi wa kituo cha afya cha ghorofa Kata ya mji mwema pamoja na mradi wa shule ya Sekondari ya mkoa wa Dar es salaam iliyoko Geza juu wilaya ya Kigamboni.