19 views 58 secs 0 comments

KAMATI YA SIASA YA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA TEMEKE

In KITAIFA
May 07, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kutoa Shukrani kwa Rais Dkt Samia kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo.ย 

Kamti ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam leo Mei 7, 2025 ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Mhe Abbas Mtemvu imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha nyingi zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo kwa ujumla Kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo.

Akiongea wakati wa Ukaguzi wa miradi hiyo Mhe Abbas Mtemvu amempongeza Mkuu wa Mkoa na viongozi wote waliochini yake kwa kazi nzuri wanayoifanya hususani utekelezaji wa mzuri wa miradi ya maendeleo yenye masilahi mapana kwa umma pamoja na ushirikiano mkubwa walionao kati ya Chama na Serikali.

Aidha kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amesema miradi yote katika Mkoa huo, itakamilika kwa wakati kwa viwango na kuzingatia thamani ya fedha “Value for Money ”

Vilevile amesema mkakati wa Mkoa kwa sasa kutokana na ufinyu wa Ardhi na ongezeko kubwa la idadi ya watu, majengo mengi ya umma ikiwemo shule, vituo vya Afya kwa sasa vitajengwa kwa Ghorofa ili kutumia vizuri Ardhi iliyopo.

Mwisho Kamati hiyo ikiwa katika muendelezo wa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo imekagua ujenzi wa Jengo la Ghorofa la Shule ya Sekondari Mangaya linalojengwa Mbagala, Maradi wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke unaojengwa Chamazi na Kituo cha Polisi cha Kisasa kinachojengwa Toangoma.

/ Published posts: 2010

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram