
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo Mei 8, 2025, amekagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa gofu chini ya Tanapa. Uwanja huo utakaokamilika mwaka huu na kuruhusu viwanja vingine vya michezo kadhaa navyo kuendelezwa, unajengwa nje kidogo ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kuibua zao jipya la utalii wa michezo.




