14 views 22 secs 0 comments

AKILI MNEMBA (AI) INASAIDIA KUBORESHA UFUNDISHAJI ILI KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

In KITAIFA
May 09, 2025

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imesaini mkataba wa mashirikiano wa miaka mitatu na Shirika lilsilo kiserikali la EdTech katika eneo la akili mnembe (AI) utaosaidia ujifunzaji na ufundishaji ili kuboresha Sekta ya Elimu nchini.

Mkataba huo umesainiwa baina ya Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba na Mkurugenzi wa EdTech Bw. Essa Mohamedali leo Mei 9, 2025 katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akieleza baada ya kumalizika kwa tukio hilo Dkt. Komba amesema, TET imepanga kufanya mafunzo ya kukuza uwezo kwa wakuza mitaala na walimu nchini kwa kutumia Akili Mnemba (AI) ili kukuza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.

Aidha, Dkt. Komba amesema lengo ni kuhakikisha idadi kubwa ya walimu nchini wanaoweza kutumia teknolojia hiyo wanafikiwa katika kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji, na kwamba katika Mtaala mpya wataingiza kipengele cha kutumia AI.

Naye, Mkurugenzi wa Tanzania AI Community, Essa Mohamedali, amesema wamefurahi kushirikiana na Taasisi ya Elimu kwakuwa wataweza kuwaongezea uwezo walimu wote nchini na kuwafanya watekeleze vizuri zaidi majukumu yao. #CloudsDigitalUpdates

/ Published posts: 2017

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram