16 views 5 secs 0 comments

Taarifa ya Pole kwa Tasnia ya Habari na Wanafamilia wa Charles Hilary

In KITAIFA
May 11, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya msiba wa father, rafiki na nguli wa habari, Charles Hilary, aliyefariki dunia alfajiri ya Mei 11, 2025. Charles alikuwa zaidi ya mwandisha, alikuwa mwalimu, kiongozi, na msukumo kwa wengi waliotangamana naye katika uandishi wa habari. Kuanzia kazi yake akiwa Radio One, BBC, Azam Media Limited hadi jukumu lake kubwa kama Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alionesha weledi, uzalendo, na heshima kwa taaluma ya habari. Kwa niaba ya wapenzi wa tasnia hii, naungana na familia, ndugu, jamaa na wanahabari wote kuomboleza msiba huu mkubwa. Tunamuombea apumzike kwa amani na milele iwe nuru yake. Urithi wake utaendelea kuishi kupitia kazi na maisha aliyogusa. Pumzika kwa amani Charles Hilary. Ulipendwa na wengi, utakumbukwa daima.

/ Published posts: 2027

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram