16 views 2 mins 0 comments

KUELEKEA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU WANANCHI MWANZA NA DODOMA WAIPA HEKO SERA MPYA YA ELIMU YA MWAKA 2024

In KITAIFA
May 11, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA


Mtaala mpya wa elimu umeanza kutumika rasmi kuanzia Januari 2024 ambao una lengo la kuimarisha ujuzi, stadi, ubunifu, na maarifa kwa wanafunzi, na kutilia mkazo zaidi mafunzo kwa vitendo (competency-based curriculum) badala ya kuzingatia kukariri. Hii inasaidia wanafunzi kuwa wabunifu, wenye stadi za maisha na tayari kwa ajira au kujiajiri.


Vipengele Muhimu vya Mtaala Mpya ni pamoja na kufanyiwa marekebisho ya Elimu ya Awali hadi Sekondari, Mitaala inasisitiza stadi za maisha, ubunifu, maadili, na ushirikishwaji wa teknolojia.


Kuelekea bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itakayowasilishwa bungeni Jijini Dodoma tarehe 12 na 13 Mei 2025, wananchi wa Mkoa wa Mwanza na Dodoma wamesema kuwa kuanzishwa kwa mtaala mpya wa Elimu kunaipeleka Tanzania kuwasaidia vijana wengi kuwa na kiwango bora cha elimu, na kuwa na uwezo wa kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo mawanda mapana ya elimu.


Wakazi wa Mwanza Abdallah Rashid, Tonny Aliphonce na Yusuph Yahaya wamesema sera mpya ya elimu nchini Tanzania ima umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya taifa, kwa sababu inalenga kuboresha ubora wa elimu, kuendana na mahitaji ya sasa ya kijamii, kiuchumi, na kiteknolojia. Sera hii mpya ilizinduliwa rasmi mwaka 2023, na utekelezaji wake umeanza kwa awamu kuanzia 2024.


Hata hivyo wameyataja maeneo muhimu Kuongeza ujuzi na maarifa ya vitendo kwa kuweka mkazo kwenye elimu ya ufundi na ujasiriamali, sera inasaidia vijana kuwa tayari kwa soko la ajira na pia kuwa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.


Kwa upande wa wakazi wa Dodoma Hassan Mkumba, Jackson Tegemeo na Elieza Mgonja wamesema kuwa Sera inasisitiza malezi ya kiutu, uzalendo, na nidhamu miongoni mwa wanafunzi, jambo linalosaidia kujenga jamii yenye mshikamano na maadili mema.


Kuhusu Teknolojia na elimu jumuishi wananchi hao wamesema kuwa Sera inachochea matumizi ya TEHAMA na kuhakikisha watoto wote, wakiwemo wenye mahitaji maalum, wanapata fursa sawa ya elimu bora ikiwa ni pamoja na kuweka mkazo kwenye kuhakikisha watoto wote wanaandikishwa shule, na kuboresha miundombinu ya shule hadi vijijini.


Kadhalika, sera hiyo ndiyo msingi wa mabadiliko ya mtaala mpya wa elimu, ambao unaendana na mazingira ya sasa, teknolojia, na mahitaji ya dunia ya leo huku ikiwa imeweka mkakati wa kuongeza idadi ya walimu, kuwajengea uwezo, na kuboresha mazingira ya shule na vifaa vya kujifunzia.

/ Published posts: 2032

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram