
CHAMA cha Wataalam wa Rasilimali watu na Utawala Tanzania(THRAPA) kinawakaribisha wataalamu wote wa rasilimali watu,wadau na utawala katika mkutano wa nne wa kitaaluma utakaofanyika Visiwani Zanzibar kuanzia Mei 20 Hadi 22,2025 ambapo mgeni rasmi ni Rais za Zanzibar na Mwenyekiti 2a Baraza la Mapinduzi Zanzibar,Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Mei 13,2025 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa THRAPA ,Christopher Kabalika Mwansasu amesema kwamba mkutano huo wa kitaaluma utaambatana na maadhimisho ya siku ya rasilimali watu dunia pamoja na mkutano wa mwaka.
Aidha,amesema mkutano huo utawakutanisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali nchini kujadili ma kubadilishana uzoefu wa kitaaluma mahala pa kazi kulingana na mabadiliko ya teknolojia duniani.
Kauli mbiu ya mkutano huo”Uwezo a nguvukazi ya baadae,inayoendeshwa na Akili Bandia”,
Hata hivyo ,Mwenyekiti Mwansasu amesema ili uweze kushiriki mkutano huo unapaswa kujisajili kwa barua pepe conference @thrapa.or.tz au kwa kupiga namba 0754004005.
Pia amesema ada za kijisajili ni laki tano kwa mwanachama wa Thrapa na kwa shilingi laki sita kwa wasio wanachama na laki moja kwa ziara ya kitaaluma.
” Njoo tujifunze Teknolojia mpya za kitaaluma na viwango vya ubora mahals pa kazi,tukuze taaluma na kujenga mtandao wa kitaaluma “,amesema
Alimalizia kwa kusema malipo yanatakiwa kulipwa kupitia akaunti namba 015C955976800 benki ya Crdb auBenki ya PBZ akaunti namba 0957345001 kwa jina la Tanzania Human Resource and administration Professionals Association