

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA imepata ugeni kutoka idara ya huduma za hali ya hewa MSD ya Zimbabwe ambao umekuja kuwatembelea na kujifunza masuala mbalimbali ya huduma za hali ya hewa Tanzania
Ugeni huo umeichagua TMA Kwa ajili ya kuja kujifunza na kutambua maendeleo na mchango mkubwa wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Katika kuimarisha huduma za hali ya hewa barani afrika

TMA
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA ilianzishwa Kwa Sheria ya mamlaka ya hali ya hewa Na.2 ya mwaka 2019 Kupitia tangazo la serikali GN 459 la Tarehe 14 juni 2019 ikiwa na jukumu la kuratibu kudhibiti na kutoa huduma za hali ya hewa Katika jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mamlaka hii inatokana na alokuwa wakala wa hali ya hewa Tanzania ulioanzishwa Kwa Sheria ya wakala (Executive Agency Act) sura namba 245 marejeo ya mwaka 2022

Kabla ya wakala wa hali ya hewa huduma za hali ya hewa nchini zilikuwa zinatolewa na iliyokuwa idara ya hali ya hewa nchini (Directorate of meteology) ambayo iliyoazishwa mwaka 1977 baada ya kuvunjika Kwa iliyokuwa jumuiya ya Africa mashariki ikiwa na jukumu la kufanya uangalizi na kutoa taarifa za hali ya hewa nchini

Kabla ya jumuiya ya afrika mashariki huduma za hali ya hewa nchini zilitolewa chini ya taasisi ya hali ya hewa iliyokuwa chini ya wakoloni
Aidha mamlaka ambayo ipo chini ya wizara ya uchukuzi Tanzania inamiliki chuo chuo Cha Taifa Cha hali ya hewa kilichopo kigoma