

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
KITUO cha Ubia kati Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPPC)kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa masuala Demokrasia (REDET) chini ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam wameandaa kongamano kwa ajili ya kujadili nafasi ya sekta binafsi na sekta ya umma kuelekea dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 .
Kongamano hilo ambalo litakuwa la wazi linatarajia kufanyika Mei 27,2025 katika ukumbi wa Maktaba katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mei,26 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia (PPPC) David Kafulila, amesema moja ya majukumu ya PPPC ni kuiwesha jamii kupata uelewa juu ya masuala ya kisera na kisheria na mipango ya Serikali katika maeneo ya ubia
“PPPC iliona ipo haja ya kushirikiana na Taasisi ya REDET ambayo imebobea katika uendeshaji wa makongamano kwa lengo la kuushirikisha umma zaidi ..
Taasisi ya REDET imekuwa ikifanya vizuri katika shughuli za makongamano na midahalo katika miongo mingi zaidi”Kafulila
Aidha amewaomba watanzania kushiriki katika kongamano hilo ambalo ni la wazi kwa ajili ya kutoa maoni na kusikiliza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya REDET, Profesa Rwekaza Mukandala amesema kongamano hilo litakuwa na mada ndogo zitakazowasilishwa.
Akitaja mada hizo ni pamoja
Dola, Masoko na Uhamasishaji wa Mitaji nafasi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.
Amesema katika mada hizo Mkurugenzi wa PPPC, David Kafulila atafanya wasilisho kuhusu dhana ya PPP na nafasi yake kuelekea Dira ya Taifa 2050 na Mwenyekiti wa REDET, Profesa Rwekaza Mukandala, ataongoza kongamano hilo
Aidha amesema kongamano hilo litaudhuliwa na Maafisa waandamizi wa serikali, wakuu wa makampuni ya sekta binafsi, wanazuoni na wawakilishi wa kada nyingine mbalimbali
Profesa Mukandala alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuhudhuria kongamano hilo la wazi ili waweze kushiriki kwenye mjadala kuhusu dhana ya PPPC na nafasi yake kwenye kutekeleza Dira ya Taifa 2050.