

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Amesema kuwa tutaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuongeza umuhimu wa matumizi ya mifumo ya biashara ya kidijitali kwa vijana wajasiriamali ili kuboresha huduma za umma na ujasiriamali Kupitia kilimo Cha mwani
Ameyasema hayo Leo 29 Mei 2025 Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe.Charlotta Ozaki Macias amesema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye warsha ya wiki ya Nordiki 2025 yenye lengo la kukuza ubunifu endelevu na matumizi ya kidijitali katika ujasiriamali kwa vijana

Amesema kuwa mila ya Nordic ya uendelevu na ubunifu—ambayo imejikita sana katika tamaduni zetu. Nchi za Nordic zimekuwa mstari wa mbele kwa muda mrefu katika biashara inayowajibika, uongozi wa kimazingira, na suluhisho za kisasa. Hivyo basi ni jambo la busara kuleta roho hiyo hapa, tukisaidia juhudi za ndani na za kimataifa kulinda sayari yetu ya pamoja.
Ameongeza kuwa uhusiano wa Nordic ni imara, kupitia wadau wa Nordic kama TechBridge na MTI, ambao wanaendesha programu ya Elevate Blue.
Basi, na tuhakikishe leo ina maana. Tuwapongeze hawa wabunifu. Tuunde mitandao. Na pia nawakaribisha kila mmoja wetu kutafakari kuhusu tabia zetu binafsi. Iwe ni kuacha kutumia chupa za plastiki kwenye matukio yenu au kushiriki katika usafi wa fukwe—kila mmoja wetu anaweza kufanya jambo kuhakikisha bahari zinadumu kwa vizazi vijavyo.

Pia Amewataka wajawasiriamali wa kilimo hicho Cha mwani kuwa waende wakazungumze na waanzilishi wa miradi.ili kutazama walichokijenga. na Kuwa na shauku ya kupata Suluhisho ambalo linalofuata la kubadili mchezo kuhusu taka baharini au uendelevu wa bahari.
“wawekezaji, wawakilishi wa serikali, na wadau: Hampo hapa kushangaa tu. Mko hapa kushiriki. Kuuliza maswali, kuhoji mawazo, na kushirikiana. Mustakabali wa maendeleo endelevu utajengwa juu ya ushirikiano unaounganisha mawazo bora na rasilimali zinazohitajika kuyatekeleza”. Amesema Macias

“wawekezaji, wawakilishi wa serikali, na wadau: Hampo hapa kushangaa tu. Mko hapa kushiriki. Kuuliza maswali, kuhoji mawazo, na kushirikiana. Mustakabali wa maendeleo endelevu utajengwa juu ya ushirikiano unaounganisha mawazo bora na rasilimali zinazohitajika kuyatekeleza”. Amesema Macias
Amesema Mwaka huu, wameangazia uendelevu, mabadiliko ya kidijiti na ubunifu kwa wanafunzi, wajasiriamali, washauri wa biashara na waendelezaji wa mazingira ya ubunifu ili kuona umuhimu wa mawasiliano katika kuongeza thamani ya ubunifu kwa vijana wajasiriamali.
Alieleza kuwa warsha hiyo imeandaliwa kwa vijana wajasiriamali kwa sababu ya kukua kwa kasi kwa matumizi ya kidijiti yanayobadilisha namna ya kuishi,kufanya kazi na kuwasiliana.

“Wakati wa kushirikiana huwa tunachunguza fursa kwa pamoja, mara nyingi kwa msaada kutoka Finnpartnership—mpango unaosaidia kufanikisha ushirikiano wa biashara na kutoa msaada wa kifedha kwa miradi ya pamoja. Ushirikiano huu ni muhimu kwa kuunda ajira, kushirikisha maarifa, na kubuni suluhisho zinazoweza kufanyika kwa kiwango kikubwa,” alisema.
Aidha alisema anaamini nguvu kubwa ya Tanzania ipo kwa watu wake hasa vijana walioelimika na wenye ndoto kubwa hivyo alitoa wito wa sekta za kidijitali zinatoa njia za ajira na ushiriki wa kimataifa kuunganisha vyuo vikuu na ujasiriamali ili kuwaanda vijana mapema na ujasiriamali.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Dkt. Amos Nungu Amesema kuwa Katika uchumi wa bluu ni eneo ambalo serikali wanaloliangalia Kwa umakini sana.”Tunawashukuru hawa wezetu Kwa kuja na hii programu”

Ameongeza kuwa ukiangalia Katika zao la mwani serikali Kupitia costech wamekuwa wakisaporti Kwa Muda mrefu kule Zanzibar ameonesha mfano kuwa mwaka juzi tuliwanunulia viboti vile vidogo Kwa ajili ya maswala ya mwani kwenye eneo ambalo tunalifanyia kazi.
“Wakati mwingine changamoto iliyopo kwamba huwatuna Ubunifu wa teknolojia peke. Yake wakati mwingine watu wanashea Ubunifu na maswala mengine”Amesema Nungu

Pia Mkufuzi wa maswala ya mwani Farhiya Elmy Amesema zao la mwani linamambo.mengi linaweza kutengeneza prasitiki Kupitia mwani sio tu sabuni unaweza kutengeneza pafyumu
Amesema vijana Wengi wamekuwa wakifanya Vitu Kwa urahisi vitu ambavyo wanajua wakifanya Leo kesho vitaingia sokoni hawako tayali kukaa chini Kwa kufanya research ya kujifunza Kwa kuleta kitu ambacho kitaleta manufaa na mabadiliko Katika nchi yetu

Aidha amewaomba serikali kuwa Sera zilizopo hazikidhi mahitaji Kwa mkulima wa mwani pia mfanyabiashara mdogo wa mwani sera waziboreshe “tukija watanzania bara hatuna sera ambayo inayouhusiana Moja Kwa Moja na uchumi wa bluu sera zitakazotengenezwa zitengenezwe Kwa mujibu ya mahitaji Kwa wafanyabiashara pamoja na wakulima Ilikuweza Kuendeleza system bilt”. Amesema Elmy