

Na Madina Mohammed
MAMLAKA ya mapato Tanzania TRA imetoa Tuzo Kwa Shirika la Taifa la nyumba NHC Kuwa kundi la mashirika ya umma na kuwa mshindi wa kwanza Kwa kuweza kulipa Kodi kwa uwaminifu
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo ijumaa 01,2023 MENEJA wa Habari mahusiano ya shirika la nyumba Ndg.Muungano Saguya Amesema anawashukuru wadau wote wa shirika la nyumba wakiwepo wapangaji wetu wanaolipa pango la nyumba na kutuwezesha kupata pesa ya kutosha na kuweza kulipa Kodi ya serikali na Kodi hiyo inaenda kuisaidia serikali Kwa kuweza kulipa huduma za jamii ikiwemo Elimu,Barabara pamoja na maji
“Kwa sisi shirika laTaifa la nyumba tutaendelea kuwa waaminifu Kwa kulipa Kodi za serikali kama inavyotakiwa Ili hatimae na sisi tuweze kuchangia Pato la Taifa na Katika kuhakikisha kwamba shirika la Taifa la nyumba linaendelea kuwa ni Moja ya mashirika mihimili yanayoweza kusaidia nchi yetu Kwa kupata mapato ya kutosha”Amesema Saguya