178 views 16 secs 0 comments

MHE KAPINGA AELEZA JUHUDI ZA SERIKALI KISAMBAZA VITUO VYA CNG NCHINI

In KITAIFA
August 27, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA Azungumzia suala la magari ya Serikali kufungwa mfumo wa CNG*

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), inajenga vituo vya kujazia gesi kwenye magari (CNG) mkoani Dar es Salaam (viwili) na mkoani Pwani (kimoja) huku TPDC ikiendelea na ununuzi wa vituo vidogo vya kujaza CNG kwenye magari vinavyohamishika ambavyo vitasimikwa katika mikoa ya Dar es Salaam (vitatu), Morogoro (kimoja) na Dodoma ( viwili).

Mhe. Judith Kapinga amesema hayo tarehe 27 Agosti, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu.

Amesema kwa  sasa kuna vituo vitano vya kujazia gesi kwenye magari katika mikoa ya Dar es Salaam (Ubungo Maziwa, Tazara na Uwanja wa Ndege), Pwani (Mkuranga)  na Mtwara (Dangote).

Kuhusu mpango wa magari ya Serikali  kutumia mfumo wa CNG amesema kuwa tayari Mtaalam Mshauri ameshapatikana  lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba suala hilo linafanyika kwa ufanisi.

/ Published posts: 1975

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram