
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Rihab Health imeandaa Kongamano la pili la Utengamao wa akili (Rehabilitation summit) linalokusudia kuendeleza ajenda ya utengamao wa Afya ya akili nchini lenye kauli mbiu ya “kuendeleza ajenda ya utengamao,kuimarisha mifumo ya Afya nchini.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Remla Shirima amezungumza na waandishi wa habari leo septemba 11 jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa kongamano hilo litawakutanisha watalam,watunga sera,watoa huduma za Afya ambapo watajadili mikakati na kuvumbua mbinu bora za huduma kwa wagonjwa wa utengamao wa akili.
“Tunalenga kuimarisha mfumo wa afya Kwa kuhakikisha huduma za utengamao zinafika Katika ngazi za msingi.za huduma za Afya na jamii”.Amesema Shirika
Pia Ameongeza kuwa “tunataka kubadilisha maarifa Kuhusu utafiti wa hivi karibuni,uvumbuzi, na mbinu Bora za kuboresha huduma za utengamao Kwa wagonjwa”.
Aidha Shirima Amesema kongamano hilo litakuwa na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa masuala ya muhimu Kama Jinsi ya kuongeza upatikanaji wa huduma za utengamao Katika maeneo ya vijijini ana yenye uhaba WA rasilimali.
“Kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi Ili kuboresha miundombinu ya huduma za utengamao na kutoa mapendekezo muhimu ya kisera na hatua za kuboresha huduma za utengamao Nchini Tanzania”. Ameongeza Shirima
Ametoa wito kwa wadau wa afya na maendeleo kushiriki katika kogamano hilo la siku tatu linatarajiwa kufanyika kuanzia 18 na kumalizika 20 septemba mwaka huu .