
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
PWANI: BANDARI Kavu ya Kwala iliyopo wilayani Kibaha mkoani Pwani ina uwezo wa kuhudumia kontena 300,000 kwa mwaka ni mara tatu ya Bandari ya Dar es Salaam, kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa.
Msigwa ameeleza hayo leo Machi 16 wakati akizungumza waandishi wa habari eneo la bandari hiyo, ambapo ameeleza kuwa bandari hiyo na zingine zinazojengwa Mwanza, Isaka, Dodoma, Tabora na mipakani mwa nchi za Burundi, Rwanda, Congo DR kutapunguza msongamano wa shehena Bandari ya Dar es Salaam.
Akitolea ufafanuzi wa ufanyaji kazi wa Bandari Kavu ya Kwala, Msigwa amesema bandari ina uwezo wa kuhudumia kontena 823 kwa siku.