
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
๐Ni kupitia Mradi wa kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo na wa kati
๐Umeme umeleta ukombozi, uzalishaji madini waongezeka Geita
Mradi wa kupeleka umeme kwa wachimbaji wadogo na wa kati, Viwanda vidogo na vya kati pamoja na maeneo ya kilimo umepokelewa kwa furaha na wananchi mkoani Geita mara baada ya kupata umeme wa uhakika katika migodi yao.
Hayo yamebaibishwa na wachimbaji wadogo wa madini wakati wakizungumza na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) mara baada ya kutembelea maeneo ya shughuli za uchimbaji madini katika eneo la Magema katika ziara iliyolenga kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa mkoani Geita.