13 views 2 mins 0 comments

NYAMGUMA MAHAMUD AIBUKA  MSHINDI HABARI ZA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

In KITAIFA
May 06, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

*๐Ÿ“ŒNi kupitia Tuzo za Uandishi wa Habari zaย  Samia Kalamu Awards*

*๐Ÿ“ŒWizara ya Nishati yatambua mchango wake*

๐Ÿ“Œ *Yamzawadia fedha taslimu, jiko linalotumia umeme kidogo, kompyuta mpakato na uniti za umeme za mwaka mmoja*

๐Ÿ“Œ *Mhandisi Mramba asema Tuzo ni kielelezo cha kuunga mkono juhudi za Rais Samia uhamasishaji Nishati Safi ya Kupikia*

Nyamguma Mahamud, Mwandishi wa Habariย  kutoka Mlimani FM ameibuka kidedea katika Tuzo za Uandishi wa Habari za Samia Kalamu Awards 2025 kupitia kipengele cha habari za Nishati Safi ya Kupikia ambapo Wizara ya Nishati imetambua mchango wake kwa kumpa zawadi mbalimbali ili kuendelea kuhamasisha utoaji wa elimu ya Nishati Safi ya Kupikia.

Hafla ya utoaji wa Tuzo hizo imefanyika jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.ย  Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mohamud amekabidhiwa zawadi zake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Mshindi huyo amekabidhiwa fedha taslimu shilingi milioni tano, kompyuta mpakato, jiko linalotumia umeme kidogo na uniti za umeme za mwaka mzima.

“Tunatambuaย  masuala aliyoyaandika katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia, kwahiyo tumemzawadia pia jiko la umeme la kisasa linalotumia umeme mdogo pamoja na umeme wa kutumia nyumbani kwake kwa mwaka mmoja,” amesema Mha. Mramba

Amesema Tuzo ya Nishati Safi ya Kupikia ni kielelezo chaย  kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katikaย  kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Samia Kalamu Awardsย  imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwa na kaulimbiu ya “Uzalendo Ndio Ujanja’

/ Published posts: 1997

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram